mapishimapishi

mapishimapishi

Jumamosi, 16 Novemba 2013

MAANDAZI YA HILIKI NA TUI LA NAZI

MAANDAZI HAYA YANALADHA SAFI SANA KWA MLAJI NI RUKSA KUONGEZA KIUNGO AU KUPUNGUZA NA ANDAZI LAKO LITABAKI NA UBORA ULE ULE MAANA SIO WATU WOTE WANAPENDA VIUNGO.
MAHITAJI

1 kikombe cha chai kikubwa
2 Amira ya chenga kijiko kidogo cha chai
1 kilo unga wa ngano
1 hiriki kijiko kikubwa cha chakula
1 kikombe cha chai tui zito la nazi na vijiko viwili vya mafuta ya kupikia ya baridi (1 kikombe cha chai mafuta ya moto kamahutumii tui la nazi )
1 chumvi kijiko kidogo cha chai
1 maji ya moto wa wastani kikombe kikubwa cha chai


Hii ni hiriki , sukari na Amira ya chenga

Weka sukari, Amira, chumvi na hiriki katika bakuli kisha weka mafuta yakupikia vijiko viwili

kisha weka tui la nazi

Kisha changanya unga wa ngano kilo moja katika bakuli

kisha weka maji ya moto katika unga

Anza kukanda unga

Kisha sukuma unga mpaka upate unene wa saizi ya andazi unalotaka 

Kisha kata andazi kwa saizi ya andazi la ukubwa unaotaka

Haya ndio maandazi mabichi baada ya kukatwa tayari kwa kuchomwa acha yaumuke kwa dakika 10 ili utakapochoma yasijae mafuta ndani

Weka mafuta ya kupikia katika kikaango kisha yapate moto wa wastani yasiwe yamoto sana maandazi yakaungua pia hayataiva ndani


HUU NDIO MUONEKANO SAFI WA MAANDAZI YA HIRIKI NA TUI LA NAZI ENJOY NA FAMILIA YAKO KWA CHAI YA JIONI AU CHAI YA ASUBUHI KWA KITAFUNWA SAFI NA SALAMA MAANA HAKINA MAFUTA MENGI PIA CHUMVI INAAIDIA KUKIMBIZA MAFUTA KATIKA UNGA.CHANZO ACTIVE CHEF

JIFUNZE KUTENGENEZA KITAFUNWA HIKI CHA MCHANGANYIKO WANDIZI MBIVU MGANDO NA CHOCOLATE


KWA RECIPE NA UPDATE ZA MAPISHI CLICK LIKE active chef kwenye facebook.com
 KITAFUNWA HIKI CHA MCHANGANYIKO WA NDIZI MBIVU MGANDO NA CHOCOLATE NA MCHANGANYIKO WA KARANGA NI RAHISI SANA KUANDAA
 
MAHITAJI
 
 3 pc ndizi mbivu
240 gram Semi-Sweet Chocolate Chips ( Vipande vya chocolate)
2 Kijiko kikubwa chachakula siagi iliyoyeyushwa
3 Kijiko kikubwa chachakula mchanganyiko wa karanga aina yeyote utakayokuanayo mfano (Almonds, Pistachios, Pecans, Hazelnuts, Walnuts, karang au korosho), weka zote au chagua uzipendazo tu.

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPA CHINI
Muda wa maandalizi : Dakika 15
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 4 vipande 15 hadi 20

 
 
Kata kata ndizi katika vipande vidogo vidogo mfano kama muonekano kwenye picha.
 
 
Chukua alluminium foil kisha ifunike katika sahani pan au tray vizuri na upande juu yake vipande vya ndizi mbivu vilivyokwisha katwa.
 
 
Kisha chukua cocktail forks au uma ya plastic zinapatiana katika supermarket pia unaweza weka chochote kitakachokua rahisi kushika . Kisha zigandishe kwenye friza kwa masaa 2 au mpaka zitakapo ganda tu toa.
 
 

Wakati unaweka katika friza muda huo huo anza kukaanga pamoja karanga za mchanganyiko ulionao .
 
 
Zikaange tu kwa wastani zinukie harufu safi kisha zitoe na uzikate kate katika vipande vidogo na ziweke pembeni  zipoe.
 
 
Baada ya ndizi kuganda sasa Chukua sufuria dogo weka maji robo kisha chukua akuli ya kioo kubwa na uweke juu yake acha maji yachemke kisha weka mchanganyiko wa siagi na chocolate chips ndani ya bakukuli ya kioo juu ya sufuria. Kumbuka kuendelea kukoroga mpaka siagi yote iyeyuke na chocolate yote iyeyuke na kua laini safi kabisa.

Pia unaweza tumia njia mbadala ambayo ni microwave lakini unatakiwa uwe mzoefu sana kwani unaweza zidisha muda wa kuyeyusha ikawa mbaya.
 
 
Toa ndizi zilizoganda katika friza, chovya kwenye mchanganyiko wa siagi na chocolate.
 
 
Kisha toa unaweza mwagia mchanganyiko wa karanga kwa juu yake au unaweza kuroll
 
 
KIsha unairudisha kwenye ile sahani ya badidi mpaka ikauke vizuri.
 
 
Kumbuka pia unaweza tumia chocolate hata zapaketi kama utakosa chocolate chips. Endapo itakua imebaki chocolate sauce unaweza itunza kwa kufunika na kuweka jikoni katika kabati kwa muda wa mwezi mmoja na isiharibike na sio kwenye  fridge. Waandalei familia watafurahia au tengeneza kwa biashara.CREDIT ACTIVE CHEF
 

JIFUNZE KUTENGENEZA KEKI HII YENYE MCHAGANYIKO WA MATUNDA


RECIPE SAFI KABISA YA KEKI HII YA TUNDA AINA YA CHUNGWA 
MAHITAJI
420 gram unga wa ngano
240 gram Sukari
2 kijiko kidogo cha chai Baking Powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
120 gram siagi au Vegetable Oil
240 gram juice ya chungwa
1 chungwa kwaruza ganda lake
2 pc ute mweupe wa yai
2 kijiko kikubwa cha chakula Icing sugar
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Chukua bakuli safi kavu kisha weka unga wa ngano, sukari, baking powder pamoja na chumvi



Kisha weka juisi ya machungwa pamoja na vegetable oil au siagi itategemea unachopenda au aina ya mafuta uliyonayo tumia mchapo piga mpaka ilainike.


Chukua bakuli nyingine safi na kavu weka ute mweupe wa yai kasha piga mpaka ilainike na upate povu kama muonekano katika picha.


Kisha chukua ule mchanganyiko wa chungwa mwagia pole pole kwenye povu la ute mweupe na tumia mwiko kukoroga pole pole ichanganyike fanya hivyo mpaka mchanganyiko wote umalizike.


Paka mafuta mazito pembeni mwa chombo cha kuokea keki yako na kasha mwagia mchanganyiko wako wa keki kwenye chombo cha kuokea.


Bake kwa muda wa saa 1 kwenye oven ambayo tayari inamoto wa wastani, kama huna uhakika tumia toothpick choma kati kati ya keki ikitoka kavu basi kekei imeiva na ikitoka na uji basi bado haijaiva ongeza muda.


Ikishaiva toa nje ya chombo cha kuokea kwadakika 10, kisha mwagia kwa juu icing sugar



MUONEKANO MZURI WA KEKI FURAHI NA FAMILIA.CREDIT ACTIVE CHEF

JIFUNZE KUTENGENEZA MCHANGANYIKO WA YAI LA KUKAANGA NA CHEESE


KAA TAYARI KWA KUJIFUNZA JINSI YA KUKAANGA YAI KWA KUCHANGANYA NA CHEESE
 
MAHITAJI
2 pc yai vunja tenga ute mweupe tu
1 pc yai Zima usilitenganishe
2 kijiko kidogo cha chai maji safi
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
60 gram Gruyere Cheese au Cheddar cheese
1 fungu Chives

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Vunja mayai 2 kwenye bakuli safi hakikisha unaweka ute mweupe tu kasha vunja yai moja Zima mwagia katika bakuli ulilitenganishe kasha weka chumvi na pili pili manga. Tumia mchapo kupiga piga ichanganyike

Kisha weka maji safi au unaweza tumia maziwa badala ya maji. Ukitaka yai lako liwe fluffier au spongy basi tumia maji.

Hutakiwi kupiga piga sana maana utasababisha mapovu kama unavyoona kwenye picha hii haitakiwi. pia unaweza kutumia uma kwenye kupiga piga na mchanganyiko wako ukawa safi. Unaweza kuweka hebs ya aina upendayo mfano parsley au korienda au chives

Weka kikaango katika moto kwa muda kiasi ipate moto. Kisha mwagia siagi ukiona imeaanza foaming and sizzling basi moto up safi. Tumia vijiko viwili vidogo vya chai siagi kasha mwagia mchanganyiko wako wa yai kwenye kikaango.

Kumbuka kulivuruga vuruga yai kwa sekunde 6 hadi8 ili liweze kuiva haraka upande wa chini

Kisha lisambaze vizuri na uliache liweze kuiva 
 
Baada ya dakika chahe utaona yai lote mieshakauta ute na kua na muonekano kama kwenye picha Zima jiko.

Mwagia  cheese kwa kufata mstari kati kati ya yai kama muonekano katika picha. Kumbuka usimwagie kwenye yai lote.

Chukua upande wa kwanza funika yai lako kisha chukua upande wa pili na ufunike pia na kupata umbo lionekanalo katika picha.

Ukilikata yai lako baada ya kuiva utaona cheese inamwagika ooooh safi sana. See that cheese oozing out from the middle?
 
    Unaweza ongeza ladha ya yai kwa kuweka vilivyotajwa hapo chini 
Crumbled Goat Cheese, sautéed shallots and fresh(or dried) thyme
Grated Emmentaler, sautéed Mushrooms and Spinach
Caramelized Onions, Crisped cubed Tempeh and fresh Marjoram
Grated Gouda and lightly stir fried thinly sliced (on the diagonal) Asparagus
 
Maji: Sio lazima kutumia maji unaweza tumia maziwa na utumiaji maziwa unasababisha creamier texture wakati ukitumia maji inasaidia  fluffiness kwenye yai.CREDIT ACTIVE CHEF

 


JIFUNZE KUTENGENEZA MTINDI FRESH AU YOGURT


RECIPE SAFI KABISA YA KUTENGENEZA MTINDI FRESH UKIWA NYUMBANI AU HOTELINI KWA URAISHI SALAMA NA HARAKA ZAIDI
MAHITAJI 1 lita ya maziwa mabichi
100 gram mtindi uwe fresh au wa kopo
 
MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA Aina ya maziwa.  Aina hizi za maziwa unaweza tumia Goat Milk, Full fat milk, Pasteurized Milk, Homogenized Milk, Raw Milk, 2% Milk, 1% Milk, Fat free] kumbuka aina ya maziwa utakayotumia na matokeo yake yatakuwa tofauti maziwa yakiwa na mafuta kiasi ndio na mtindi wako utakua mzito  
Thermometer ni lazima?: Sio lazima kabisa kwani bibizetu sikumbuki kama walikua wanatumia kumbuka maziwa hayatakiwi kuwa yamoto yanatakiwa kuwa yavugu vugu weka kwenye kiganja kupima kama tayari yanauvugu vugu kabla ya kuweka mtindi fresh.

Mtindi wangu haujawa bado ni maziwa tatizo nini?  sababi ya kwanza unaweza ukawa umetumia maziwa ya  UHT (Ultra High Temperature) processed milk. ingawa pia unaweza kutengenezea yogurt ikiwa utafata vipimo na maelezo vizuri,  Sabau ya pili unaweza ukawa umetumia mtindi ulioharibika katika kuchanganyia na sababu ya tatu ni kutochemka kwa maziwa kwa joto la 105-110 F temperature au umechanganya mtindi kwenye maziwi yamoto sana au yabaridi sana.
 
JINISI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Muda wa maandalizi : Masaa 4 hadi 8
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 4


Chemsgha maziwa mabichi kwa nyuzi joto 110F. Ukiyachemsha mziwa katika joto la 110F, bado maziwa yanakua katika ladha ya uhalisia ya ubichi.
Note: sio lazima kutumia maziwa mabichi kwa recipe hii


Note: kama utataumia maziwa ambayo yameshachemshwa basi kumbuka kuyapoza mpaka joto lifikie 110F before the next step.


Nilibakisha yogurt kiasi ndio naitumia tena kama huna unaweza nunu mtindi fresh na ukatumia katika hatua inayofuata baada ya kuchemsha maziwa.

Kisha mwagia mtindi huo ndani ya maziwa .

Stir and whisk it so that it dissolves and is well distributed  throughout.

Funika na mfuniko hakikisha kua joto lilikua ni 105F to 110F . Ili iweze kuganda na kuset haraka unatakiwa uwashe oven kwa dakika mbili kasha Zima halafu weka sufuria yako itachukua masaa 3 hadi 5 kuganda na kuset,kwasehemu zenye joto kama Tanga , Dar es salaam, Zanzibar na mtwara unaweza weka tu pembei ya jiko na baada ya masa 5 ikawa imeganda vizuri kabisa sababu ya hali ya hewa na mgandamizo wa hewa wa juu.
 
See that set yogurt with a yellow layer on top?.

Kwasababu maziwa tuliotumia ni fresh basi cream inakuja juu na nzito kabisa.

 Ukitaka mtindi wako uwe mzito basi chukua kitambaa na chuza maji kisha itabakia cream nzito nasfi kabisa.


Weka katika bakuli na unaweza kuongezea ladha za matunda mfano embe, chungwa, nanasi au ndizi familia au wateja wako wakafurahia sana.credit active chef blog