mapishimapishi

mapishimapishi

Alhamisi, 19 Desemba 2013

JIFUNZE KUTENGENZA KEKI YA NDIZI MBIVU


RECIPE SAFI KABISA NA JINSI YA KUETENGENEZA KEKI YA NDIZI MBIVU

MAHITAJI
360gram unga wa ngano
180 gram sukari
1 kijiko kidogo cha chai baking powder
1/2 teaspoon baking soda
1/4 kijiko kidogo cha chai chumvi
4 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya karanga
6 ndizi za kuiva zigandishe kwenye freezer
1/2 kijiko kidogo cha chai vanilla essence
100 gram korosho au karanga za kuoka

Kwajili ya Honey Cinnamon Frosting (Sio lazima)
300 gram Icing sugar
120 gram siagi isiyo na chumvi iyeyuke kama mafuta mgando yakupaka
1 kijiko kikubwa cha chakula Asali
1/8 kijiko kidogo cha chai unga wa cinnamon (Mdarasini)
  Na Chef Issa Kapande
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI


Washa oven yako katika moto wa 350 degrees. Chukua backing tray yenye mashimo 12 ya muffin kisha weka zile karatasi maalumu za kuokea au paper liners. Chukua bakuli safi kavu kasha changanya Unga wa ngano, sukari, baking powder na chumvi salt.


Kisha toa ndizi zilizokua katika freezer ziweke nje kwa dakika 20 zitoe barafu.
 
Menya ndizi na ziweke kwenye blenda saga mpaka upate rojo safi kabisa.

Kisha mwagia mchanganyiko wako wa ndizi kwenye mchanganyiko wa unga pamoja na mafuta ya karanga na vanilla.

Tumia mwiko kuchanganya pole pole mpaka mchanganyiko wako uchanganyike vizuri.
 
Chukua kijiko kikubwa au mwiko kisha anza kumimina pole pole kwenye mashimo ya muffin.

Hakikisha umegawanya vizuri mchanganyiko wako utimie maffin 12 na ujazo uwe kama muonekano katika picha.

Oka ukiweka toothpick kati kati ya muffin na ukitoa inatoka safi bila uji uji,  kwa dakika 25 hadi 30.

Zitoe muffin zako zikiwa bado katika zile karatasi maalumu za kuokea na weka zipoe ktk wire rack.

Kwajili ya Frosting ya asali:  Kisha chukua Asali, sukari ya unga, unga wa mdarasini na siagi ilyoyeyuka kama mafuta mgando ya kupaka.

Nakushauri kutumia mixer ya umeme, piga kwadakika 4 hadi 5 mchanganyiko utakua laini.

Unaweza tumia walnut au karanga au korosho chaguo ni lako kisha zi chop chop.
 
Nakushauri tumia piping bag kupambia kwajuu. Unaweza tumia hata kijiko kupambia.
 
Sio lazima kuweka frosting lakini ukiweka inapendeza zaidi na utamu ndio unazidi na harufu safi ya mdalasini.

Mafuta ya karanga yanasaidia sana keki yako isishike na iwe rahisi kutoa wakati wa kula pia kwa wenye matatizo ya kiafya hasa sukari usitumie frosting.

Unaona vizuri spongy kwa ndani? Ipo fluffy, light and very flavorful.

We enjoyed them the day I made them (for evening tea or breakfast the next morning after warming them up slightly. It makes a great breakfast too.
 
Mwagia kwa juu hizo karanga  zitaongeza ladha safi pia


Kama mchanganyiko wako utakua mzito basi unaweza ongeza maji ya vugu vugu 60 gram usitumie maziwa yataifunika ladha ya ndizi.

RECIPE SAFI SANA YA KITAFUNWA HIKI CHENEY LADHA YA NDIZI, MDARASINI NA ASALI

JIFUNZE KUTENGENEZA ENCHILADA YA KUKU NA MAHINDI MABICHI



KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA ENCHILADA YA KUKU NA MAHINDI MABICHI PIA HISTORIA YAKE

MAHITAJI
12pc tortilla za mahindi
480 gram nyama ya kuku
480gram mahindi mabichi (sweet corn) 
480 gram shredded cheese (cheddah)
1 kopo kubwa la enchilada sauce
sour cream (Sio lazima nikwajili ya kupambia)
na chef issa Kapande
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI







JIFUNZE KUTENGENEZA PANCAKE SAFI NA NZITO KWAJILI YA KITAFUNWA



RECIPE SAFI KABISA YA PANCAKE NZITO NA SAFI KWA KITAFUNWA CHA ASUBUHI, MCHANA AU JIONI
 
MAHITAJI
240 gram unga wa ngano
3 kijiko kikubwa cha chakula sukari (white sugar)
1/2 kijiko kidogo cha chai Baking Soda
1/2 kijiko kidogo cha chai Baking Powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
360 gram cups fresh cream
1 pc yai
kijiko kikubwa cha chakula butter  au (Siagi)
kijiko kikubwa cha chakula vanilla 
muuandaaji ni chef issa kapande
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
Chukua bakuli safi kavu kasha changanya unga wa ngano, sukari, chumvi, baking powder na baking soda.

Kisha chukua bakuli nyingine safi na kavu kasha changanya pamoja mayai, vanilla essence, siagi na fresh cream kama huna unaweza tumia maziwa badala yake.

Kisha chukua mchanganyiko wa mayai na maziwa mwagia kwenye mchanganyiko wa wa unga na koroga pole pole. Kisha weka pembeni acha kwa dakika 5 hadi 10 sio lazima lakini kama ukiweka kwa muda huo itulie pancake yako itatoka vizuri sana.

Chukua non stick pan, mwagia mafuta kiasi hakikisha jiko lako halina moto mkali au moto mdogo . Medium heat is perfect for pancakes. chukua kijiko kikubwa au upawa mmoja chota na mwagia katika kikaango.

Ukitaka kujua recipe umeipatia au jiko lako linamoto safi basi utaona  holes au bubbles zinatokea kwa juu sasa ujue ndio na muda wa kugeuza umefika igeuze pancake yako. Kawaida inachukua kama 50 sekunde mpaka dakika.

Turn the pancakes when golden brown and let it cook for another few seconds or until done.

Angalia pancake ilivyochambuka safi sana na nzito ukila unashiba

Hapa familia lazima ijiume videle bwana


Tumia kitambaa kizito au towel kuzifunika wakati unaendelea kupika ili zibaki na moto kwani zinapendeza kuliwa zikiwa za moto wakati wa kula unaweza mwagia maple syrup oooooh ladha yake itakua baabkubwa (a must! Dont even think of skipping it) and feel heaven coming down :) Pia unaweza kutumia chocolate sauce au strawberry syrup.

JIFUNZE KUAMSHA LADHA KWENYE WALI ULIOPIKWA NA UKALALA





MAHITAJI
700 gram za wali uliolala ( Kiporo)
1pc kitunguu maji kikubwa
5 pc nyanya za kuiva
1 kijiko kidogo cha chai dengu
1/4 kijiko kidogo cha chai pili pili manga
1/4 kijiko kidogo cha chai Turmeric powder
kijiko kidogo cha chai Sambar Powder, 
1 pili pili moja kavu (siolazima)
kijiko kidogo cha chai mafuta ya kupikia
kijiko kidogo cha chai siagi
Majani ya Curry kiasi
majani ya giligilani kiasi
na chef issa
KUJIFUNZA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI