mapishimapishi

mapishimapishi

Jumatano, 24 Julai 2013

JIFUNZE KUPIKA SAMAKI KATIKA OVEN KWA KUTUMIA FOIL


 
NI RAHISI, NAFUU NA HARAKA SANA KUANDAA AINA HII YA MAPISHI YA SAMAKI KWA KUTUMIA FOIL NA KUOKA KATIKA OVEN LAKINI SAMAKI ATATOKA KAMA AMECHEMSHWA NA AKIWA NA LADHA SAFI SANA BILA YA KUPOTEZA VIRUTUBISHO VYOTE MUHIMU.
 
MAHITAJI
1pc kitunguu maji kikubwa
1 pc limao kubwa
5 gram binzali
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
1 pc pili pili hoho kubwa
50 gram tomato pest ( nyanya ya kopo)
kipande cha foil kutokana na ukubwa wa samaki
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
 
Huu ni muonekano wa samaki akiwa mbichi tayari umeshamsafisha vizuri kwa maji baridi na mapishi haya unaweza tumia kwa samaki aina ya sato, sangara, kibua, change, jodari au kole kole na akaiva na ladha safi kabisa.

 
Katika picha unaona mchanganyiko wa vitunguu, pilipili hoho, maji ya limao, binzali, chumvi, pili pili manga na nyanya ya kopo baada ya kuchanganya pamoja kasha mpakae samaki pande zote mbili ulizompasua ili mchanganyiko huu uingie vizuri katika nyama kasha mabaki ya huo mchanganyiko mjazie tumboni kisha mfunike vizuri na foil muweke katika oven tayari ikiwa na moto.
 
Jana mchana niliporudi nyumbani niliandalia samaki aina ya sato pamoja na maharage ya Nazi na ugali wa mahindi nipo ulaya lakini na kula chakula nilichokizoea nyumbani Tanzania na kwa ladha na ubora ule ule.
 
 
 
Unaweza kumpika katika oven kwa dakika 30 kwenye moto wa degree 200 hadi 250 pia kwa mtindo huu unaweza kumchoma katika jiko la mkaa akiwa hivi hivi katika foil na akaiva safi kabisa
 
 
 
Baada ya nusu saa samaki wako atakua ameiva na atakua na muonekano kama huu na ladha safi sana
 

 
Hapa sasa ndio nilikua namfunua vizuri tayari kwa chakula cha mchana

 
Hata kama samaki amekaa kwenye friza kwa muda mrefu mchanganyiko huu wa mboga majani limao na viuongo vinasaidia sana kuamsha ladha ya samaki wako pika familia ifurahie.
 

JIFUNZE VITAFUNWA MBALI MBALI WAKATI HUU WA MWEZI MTUKUFU


 
 
KAA TAYARI KWARECIPE NYINGI TOFAUTI ZA VITAFUNWA KWA MWEZI HUU MTUKUFU WA RAMADHANI
 
 
HAPO CHINI NI KITAFUNWA CHA MCHANGANYIKO WA MBEGU ZA UFUTA MAELEZO YANAKUAJA BAADAE KIDOGO NA PICHA ZAIDI
SOURCE ACTIVE CHEF BLOG


 

 





 

 

 
 
 



JIFUNZE KUTENGENEZA KITAFUNWA HIKI CHA UNGA WA MAHINDI NA MAJNI YA KITUNGUU


 
KATIKA MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VITAFUNWA WAKATI HUU WA MFUNGO KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA KITAFUNWA HIKI CHENYE MCHANGANYIKO WA UNGA WA MAHINDI NA MAJANI YA KITUNGUU
SOURCE ACTIVE CHEF BLOG
 
 














JIFUNZE NAMNA YA KUPIKA KEKI AINA TATU ZA MAZIWA



KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA KEKI HII YA MAZIWA AINA TATU

MAHITAJI

240 gram unga wa ngano
1-½ kijiko kidogo cha chai Baking Powder
¼ kijiko kidogo cha chai Salt
5 yai zima, kisha tenganisha ute wa njano na mweupe
240gram Sukari, gawa nusu pembeni
1 kijiko kidogo cha chai Vanilla
30 gram maziwa ya maji
1 kopo la Evaporated Milk
1 kopo la Sweetened au Condensed Milk
60gram za cream nzito kabisa ( Heavy Cream)


KWAJILI YA ICING:


1 kijiko kikubwa cah chakula Heavy Cream, kwajili ya kupambia
3 kijiko kikubwa cha chakula sukari nyeupe ya unga
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEKEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : 1 mpaka masaa 2

Muda wa mapishi : 30 dakika mpaka saa 1
Ukubwa na Idadi : utapata cake 2 


Washa kwanza oven kwa moto wa 350 degrees. Kisha chukua tray yenye size hii 9 x 13 inch unaweza paka siagi au ukaspray. Kisha chukua unga changanaya na baking powder pamoja na chumvi katika bakuli kubwa.

Kisha chukua bakuli safi na kavu weka ute wa yai wa njano pamoja na sukari 180 gram piga kwa kutumia mchapo kwa nguvu sana au kama unatumia mashine basi weka spidi kali.

 

Hakikisha inakua muonekano huu baada ya kupiga na mshine unapata rangi ya cream.



Kisha chukua yale maziwa ya maji pamoja na vanilla kisha chukua mwiko huo na changanya pole pole mpaka vyote vichanganyike vizuri.


Kisha chukua ute mweupe wa yai (egg whites) piga tena kwa kutumia mashine kwa spidi kali mpaka uone imetoa mapovu kabisa na kuongezeka. 



Baada ya kutoa povu basi chukua sukari 60 gram na mimina katika mchanganyiko huo wa ute mweupe wa yai.


Endelea kupiga tena kwa kutumia mashine kwa spidi kali hakikisha imekua laini kabisa kama mapovu lakini isikwe kavu.



Unaona muonekano baada ya kua katika kiwango safi na imetengeneza kama milima miwili?



Chukua ule mchanganyiko mweupe wa yai changanya pamoja na mchanganyiko ule wa unga.



Hakikisha unachanganya pole pole

 


Mpaka ichanganyike vizuri kabisa.


Kisha mimina mchanganyiko wako kwenye tray ulioandaa kwajili ya kuokea hakikisha unasambaza vizuri.

 

Choma kwa dakika 35 mpaka 45 au mpaka toothpic ukitoa inabaki kavu. Mara yangu ya kwanza kuipika keki hii nilifungua oven zaidi ya mara 100 ambayo ni kosa sababu ya harufu nzuri ilioenea jikoni kila muda nahisi labda imeshaiva! Nadhani ndio maana keki yangu ilinywea hahahahaaaa! usifanye kosa hili ingawa taste yake ilikua YUMMO!



Keki yako tayari inarangi safi sana ya kahawia kisha chukua condensed milk, evaporated milk pamoja na heavy cream changanya.


Hakikisha unachanganya pole pole mpaka ichanganyike vizuri.

 

Baada ya keki yako kuiva weka pembeni ili ipoe na ikishapoa, Chukua uma na uitoboe pole pole . 


KIsha chukua mchanganyiko huo wa nmaziwa na cream mwagia juu ya keki na uruhusu ipoe kwa dakika 30. Weka kwenye friji ili ipate ubaridi kabisa isisumbue unapoipamba na icing. Chukua  heavy cream na vijiko 3 vyasukari kisha piga pamoja. 

 

Hakikisha unapiga mpaka inalainika kabisa.


Hakikisha unapakaza vizuri icing yako juu ya keki yote ili kuongeza ladha, ingawa mimi huwa nagawa nusu napaka na nusu sipaki maana sio watu wote wanapenda cream. Umeona muonekano baada kukata kipande? Unaona muonekano wa maziwa sehemu tuliokata kipande cha keki? maziwa unayoweka katika hii keki hayatabadiklisha sana keki yako iwe tepe tepe bado itakua na hali ya sponji.



Keki hii asili yake ni nchi ya spain wao wanapenda sana kupambia kwa juu matunda aina ya peaches na cherries. Kwakua ilikua ni msimu wa maembe mi nikaona kwanini nisipambie maembe ?!


Baada ya kupaka cream kwa juu kisha pamba na maembe na kata vipande kama muonekano katika picha.CHANZO activechef



Ukitafuna utaona sponji safi kabisa na ladha safi
 


Pia hata hotelini unaweza kuuza keki hii kama chakula kitamu baada ya mlo kamili
 



Waandalie nyumbani waweze kufurahia keki hii kwa chai ya jioni au baada ya chakula.