KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA MUDA SI MREFU
MAHITAJI
500gram low fat Milk yanapatikana duka lolote la chakula
200gram tui la nazi
60 gram maziwa ya kawaida yaliyochemshwa yakapoa
1 kijiko kikubwa cha chakula Cocoa powder
1/4 kijiko kidogo cha chai Vanilla
50 gram fresh whipped cream (sio lazima)
vipande vya Chocolate (sio lazima)
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Muda wa maandalizi Dakika 15
Muda wa kutengeneza: Dakika 15
Idadi ya walaji: Watu 3
Ujazo baada ya kuandaa : 600 ml
Katika kikaango mimina maziwa aina zote pamoja na tui la nazi.
Chemsha mchanganyiko huu kwa moto mdogo, hakikisha unakoroga pole pole.
Kisha mimina unga wa cocoa na uendelee kukoroga
Hakikisha unaendelea kukoroga ichanganyike vizuri.
Toa katika moto kisha mimina vanilla katika mchanganyiko wako.
Mchanganyiko wako utakua mziko kiasi mpatie mnywaji ikiwa ya moto juu
yake unaweza pamba na whipped cream pamoja na unga wa chocolate.
Hutaweza kusikia ladha kali ya nazi ila kama wewe ni mpenzi sana wa nazi
punguza idadi ya maziwa kisha weka nazi zaidi kwa ladha unayotaka.
Muandalie mgeni nyumbani au watoto kinywaji hiki rahisi na cha haraka
kuandaa.