mapishimapishi

mapishimapishi

Jumatano, 24 Julai 2013

JIFUNZE KUTENGENEZA HOT CHOCOLATE YA MCHANGANYIKO NAZI

 
KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA MUDA SI MREFU
 
MAHITAJI
 
500gram low fat Milk yanapatikana duka lolote la chakula
200gram tui la nazi
60 gram maziwa ya kawaida yaliyochemshwa yakapoa
1 kijiko kikubwa cha chakula Cocoa powder
1/4 kijiko kidogo cha chai Vanilla
50 gram fresh whipped cream (sio lazima)
vipande vya Chocolate (sio lazima)
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi Dakika 15
Muda wa kutengeneza: Dakika 15
Idadi ya walaji: Watu 3
Ujazo baada ya kuandaa : 600 ml

 
Katika kikaango mimina maziwa aina zote pamoja na tui la nazi.

 
Chemsha mchanganyiko huu kwa moto mdogo, hakikisha unakoroga pole pole.

 
Kisha mimina unga wa cocoa  na uendelee kukoroga

 
Hakikisha unaendelea kukoroga ichanganyike vizuri.

 
Toa katika moto kisha mimina vanilla katika mchanganyiko wako.

 
Mchanganyiko wako utakua mziko kiasi mpatie mnywaji  ikiwa ya moto juu yake unaweza pamba na whipped cream pamoja na unga wa chocolate. Hutaweza kusikia ladha kali ya nazi ila kama wewe ni mpenzi sana wa nazi punguza idadi ya maziwa kisha weka nazi zaidi kwa ladha unayotaka. Muandalie mgeni nyumbani au watoto kinywaji hiki rahisi na cha haraka kuandaa.

JIFUNZE KUTENGENEZA KEKI HII YA MCHANGANYIKO WA KOKOA BILA YA KTUMIA MAYAI


 UTENGENZAJI WA KEKI HII YA MCHANGANYIKO WA KOKOA BILA YA KUTUMIA MAYAI
 
MAHITAJI
250 gms unga wa ngano
250 gms sukari
250 gms siagi
50 gms unga wa cocoa
1 kijiko kidogo cha chai baking soda
1/2 kijiko kidogo cha chai baking powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
1 kijiko kidogo cha chai vanilla essence
250 gram pureed Mori Nu silken Tofu (Badala ya mayai 4)

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : Dakika 30 mpaka saa 1
Muda wa kupika 30 mpaka saa 1
Idadi ya walaji: Watu 4
 
Hii ni picha ya Tofu inauzwa madukani.
 
 
Washa oven katika moto wa 180 deg C (350 deg F). Paka siagi au mafuta pia nyunyizia unga kwa mbali kwenye pan  ya ukubwa huu (8″x8″), Fungua box lenye mchanganyiko wa tofu na upoige kama wewe hutumii mayai nakama unatumia mayai basi piga mayai 4 piga kwa mkono au mashine mpaka uone mapovu.

 
Weka katika chujio la chuma unga wa ngano, cocoa powder, baking powder, baking soda pamoja na chumvi.

 
Hakikisha umechekecha vizuri na kisha weka pembeni.

 
Chukua siagi na sukari pia piga kwa mashine au mchapo changanya na vanilla essence.

 
Chukua mchanganyiko wa tofu au mayai weka katika mchanganyiko wa siagi na sukari. 
 
 
Tumia mchapo au mashine chapa mpaka uchanganyike safi kabisa mchanganyiko wako.
 
 
Sasa mimina mchanganyiko wa unga pole pole katika mchanganyiko wa siagi na mayai au tofu

 
Kisha endelea kupiga kwa mchapo au mashine mpaka mchanganyiko wako uchanganyike vizuri.

 
Kama mchanganyiko wako umekua mzito basi unaweza mimina pole pole maziwa huku ukiendelea kuchanganya.

 
Kisha mimina mchanganyiko wako mzito katika pan,

 
Hakikisha unasambaza vizuri kwa juu iwe na muonekano mzuri kabisa.
 
 
Kisha choma kwa dakika 45 mpaka 5 itakua imeiva. ( oven yangu inachoma kwa dakika 32 tu )

 
Huu ndio muonekano wa keki baada ya kuiva, hapa nimeiweka ili ipoe.
 
 
 
Weka keki yako katika tray yake kisha mwagia sukari ya unga au icing sugar kwa juu kuongeza mvuto. Unaona muonekano safi kabisa. Pika kwa biashara au kitafunwa nyumbani.
 

JIFUNZE KUTENGENEZA YAI JICHO LA NG'OMBE NA KIPANDE CHA MKATE


 
RECIPE SAFI KABISA YA KUTENGENEZA KITAFUNWA HIKI KWA WAKATI WA MAPUMZIKO YAHA MAREFU.
 
MAHITAJI
 
1 Yai
1 kipande cha mkate
1/2 kijiko kidogo cha chai siagi
5 gram chumvi
2 gram pili pili manga
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
 
Chukua kipande cha mkate kunja nusu kisha kata mduara kati kati.

 
Huu ndio muonekano wa mduara baada ya kukata

 
Chukua brush na kisha paka pande zote mbili siagi.

 
Chukua kipande cha mkate kisha weka katika kikaango chenye moto wa wastani ili isiungue.

 
Kisha pasua yai na mimina kati kati ya mkate

 
Kisha nyunyizia chumvi na pili pili manga kwa juu ya yai nali mkate.

 
Baada ya dakika 3 hadi 4, upande mmoja uta.kua umeiva geuza upande wa pili

 
Upande wa pili pika kwa dakika 2 tu utakua umeiva pia.


HUU NI MUONEKANO WA MKATE JICHO LA NG'OMBE UKIWA UMEIVA WAANDALIE FAMILIA WAFURAHIE.

JIFUNZE JINSI YA KUPIKA MKATE HUU MWEUPE


JIFUNZE KUTENGENEZA MKATE HUU MWEUPE NI RAHISI NA NAFUU KUANDAA ONYESHA UJUZI WAKO KATIKA FAMILIA
 
MAHITAJI
 
1 kg unga wa ngano
2 kijiko kidogo cha chai chumvi
240 gram maziwa ya maji ya vugu vungu
60 gram maji ya vugu vugu
2 kijiko kikubwa cha chakula siagi, iyeyushe
3 kijiko kikubwa cha chakula asali
2 kijiko kidogo cha chai amira ya chenga

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
Muda wa maandalizi : Masaa 2 hadi 4
Muda wa mapishi : Dakika 30 hadi saa 1
Idadi ya walaji : Watu 4
Ujazo : Unapata mkate wenye 9-inch
 
 
Chukua robo tatu ya unga pamoja na chumvi kisha chukua mchapo na uchanganye. 

 
 Chukua bakuli safi kavu kisha changanya maziwa, majina, siagi, chumvi pamoja na amira. Hakikisha joto la maziwa na maji liwe 110 degrees.

 
 Mimina mchanganiko wako wenye maziwa katika unga.

 
Anza kukanda pole pole 

 
Hapa mchanganyiko wako umeshaanza kushikana. 

 
Chukua mchanganyiko wako kisha weka juu ya meza hakikisha umemwagia unga kwa juu endelea kukanda vizuri kwa dakika 10.

 
Kama unafikiri mchanganyiko bado una maji maji, basi chukua robo ya unga iliobakia tumia kijiko kikubwa cha chakula ongeza kimoja kimoja epuka kuweka unga wote ukazidisha.

 
Chukua bakuli safi na kavu, kisha lipake mafuta na weka mchanganyiko wako katika hiyo bakuli. 

 
KIsha tumia plastic na funika weka sehemu yenye joto, jikoni kuna joto.

 
Hakikisha mchanganyiko wako umeongezeka mara 2, ndani ya dakika 40 mpaka 50. 

 
Kisha chukua mchanganyiko wako ukande vizuri na weka katika chombo chako cha kuokea kiwe cha chuma au cha kioo kama changu chenye ukubwa wa  8.5 X 4.5 X 2.5 (1.5 Lita).

 
 Kisha funika tena kwa plastic

 
 Weka pembeni kwa dakika 20 mpaka 30 itakua imeshaumuka vizuri kama unavyoona katika picha weka katika oven.

 
 Kumbuka oven yako unatakiwa uiwashe kabla katika joto la 350 degrees, ukishaweka unga katika oven unaweza rushia maji kidogo ili kuweka mvuke utakao saidia kuweka rangi nzuri ya brown na kua na gamba gumu. Oka kwa dakika 40 mpaka 50 mkate wako utakua umeiva.

 
Toa mkate wako katika pan, hamishia katika wire rack, ili mkate uweze kupoa.

 
Kata kata vipande na wapatie walaji, unaona mkate ulivyochambuka. 

 
Unaweza ukavuta picha huu mkate ni mtamu kiasi gani ukishapaka siagi kwajuu? au ukipaka jam pia? Ni mtamu sana sana.

JIFUNZE KUPIKA YA MUFFIN YENYE MCHANGANYIKO WA VIPANDE VYA CHOCOLATE NA KARANGA


 
RECIPE SAFI KABISA YA MUFFIN YENYE MCHANGANYIKO WA VIPANDE VYA CHOCOLATE NA KARANGA NI TAMU RAHISI NA NI NAFUU KUANDAA

MAHITAJI

250 gram siagi laini
250 sukari
2 mayai
250 gram plain yogurt
1 kijiko kidogo cha chai vanilla
500 gram  unga wa ngano
1 kijiko kidogo cha chai baking soda
1/2 kijiko kidogo cha chai baking powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
180 gram vipande vya chocolate
1 kijiko kidogo cha chai cinnamon powder
4 kijiko kikubwa cha chakula karanga za kuoka
2 kijiko kikubwa cha chakula sukari ya brown
60  gram vipande vya chocolate
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
Muda wa maandalizi : Dakika 30
Muda wa mapishi : Dakika 30
Idadi ya keki : 12 Muffins
 
Katika bakuli changanya sukari na siagi pamoja.
 
Kisha mimina mayai pole pole endelea kuchanganya katika mchanganyiko wa sukari na siagi.
 
Kisha ongeza yogurt na vanilla na uchanganye ichanganyike vizuri.
 
Kisha chukua bakuli safi na uchanganye unga wa ngano pamoja na baking soda, baking powder na chumvi.
 
Kisha chukua mchanganyiko wa unga kisha mimina polepole katika mchanganyiko wa mayai.
 
Kisha mimina vipande vya chocolate na uendelee kuchanganya polepole.
 
KIsha chukua tray ya kuokea na weka vikombe vya karatai kisha mimina mchanganyiko wako 2/3 hakikisha isijae kabisa.
 
Kisha chukua bakuli kavu weka vipande vya chocolate vilivyobakia, cinnamon powder na karanga changanya pamoja.
 
Kisha mwagia kwa juu mchanganyiko huo kwenye tray ya kuokea izibe ile nafasi iliyobakia.
 
Hakikisha oven unaiwasha dakika 5 kabla ya kuoka Choma katika ovena katika moto wa 350F kwadakika 20 had 30. Poza keki zako kwa dakika 5 kabla ya kuzitoa katika pan.
 
Naimani ukizieweka sehemu nzuri ukafunika safi zisiguswe na wadudu zinaweza kukaa kwa siku tatu bila ya kuharibika!