
PUNGUZA KILO MOJA Group,kuku huyu anawafaa sana.Hakuna kuongeza mafauta,na utatumia tangawizi na applecider .(Naamini mnafahamu umuhim wa viungoo hivi)
Mahitaji
- Kuku kilo 1
 - Vitunguu saumu kijiko 1 cha chakula-kata vipande vidogo
 - Tangawizi ½ kijiko cha chai
 - Basil kijiko 1 cha chai
 - Parsley kijiko 1 cha chai
 - Pilipili manga ½ kijiko cha chai
 - Curry powder ½ kijiko cha chai
 - Apple cider Vinegar vijiko 3 vya chakula
 - Chumvi kwa ladha upendayo
 
1.Katika sufuria weka Nyama,chumvi ,pilipilimanga na tangawizi,Changanya vizuri .kisha weka curry powder,Vitunguu saumu ,Basil na parsley kwa juu,usichanganye.Funika na chemsha kwa moto mdogo
- Viungo vilivyokaa juu havichanganywi kwani hushika chini na kuungua kwa haraka
 - Usiongeze mafuta katika pishi hili
 
Kama familia inawatoto,Usiweke pilipili manga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni