MAHITAJI
1 kijiko kidogo cha chai Kosher Salt
1 kijiko kidogo cha chai Freshly Ground Black Pepper
1 kijiko kidogo cha chai Onion Powder
1 kijiko kidogo cha chai Garlic Powder
1 kijiko kidogo cha chai Dried Parsley Flakes
Na Chef Issa Kapande
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Changanya viungo vyote kwa mara moja kisha mwagia juu ya vifua vya kuku
Ukitaka upate harufu na ladha safi toka katika viungo hivi hakikisha
umeasha moto na kikaango kipate moto wa kutosha kisha mwagia mafuta
yakupikia yakutosha na mwagia pia viungo vilivyobakia kwenye kikaango
kisha weka hivyo vifua vyakuku na upunguze moto uwe wa wastani.
Chukua mfuniko funika ila acha wazi kiasi kama muonekano kwenye picha
lengo ni kupunguza mvuke isiwe kama tunachemsha badala ya kukaanga.
Kaanga kwa dakika 3 kisha geuza upande wa pili uweze pata rangi ya
kahawia nzuri.
Baada ya kugeuza upande wa pili huu ndio muonekano wake na kisha pika
pia kwa dakika 3 na kifua cha kuku kitakua kimeiva. Kumbuka unapogeuza
upande wa pili toa na mfuniko usifunike tena.
Huu ni muonekano wa perfectly cooked and seasoned chicken breast baada
ya kukata ndani inakua laini na ladha safi kabisa sio kau kau na
kupoteza ladha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni