Kahawa.
Utafiti
umethibitisha kuwepo uhusiano kati ya ukosefu wa usingizi na matatizo ya
kiafya kama vile ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa kisukari na saratani
KINACHOSABABISHA UKOSEFU WA USINGIZI
Ingawa
msongo wa mawazo nao unatajwa kuchangia mtu kukosa usingizi, lakini mlo
unaweza kuwa ndiyo sababu kubwa inayoweza kumkosesha mtu usingizi, na
hasa vyakula vitano vifuatavyo:
POMBE
Unywaji
wa bia moja ama mbili unaweza kukufanya upate usingizi haraka, hivyo
kukufanya uamini kuwa pombe inasaidia mtu kupata usingizi haraka. Ingawa
unaweza kupata usingizi haraka kwa kunywa pombe, lakini utafiti
umeonesha kuwa usingizi huwa unakata usiku wa manane, au sehemu ya pili
ya usingizi na kukuamsha asubuhi ukiwa mchovu.
KAHAWA
Inajulikana
kwamba kahawa ndiyo chanzo kikuu cha kilevi aina ya ‘caffeine’.
Inaelezwa kwamba kilevi hiki hudumu mwilini kwa muda usiopungua saa
tano, hivyo kutegemeana na wakati gani umetumia kahawa, athari zake
huweza kuonekana hadi usiku wakati wa kulala.
Hivyo
kwa mtu mwingine, hasa mwenye matatizo ya usagaji chakula tumboni (poor
metabolism), kikombe cha kahawa utakachokunywa mchana, athari zake
zinaweza kuonekana hadi usiku wakati wa kulala, kwani unaweza kujikuta
unapoteza usingizi wakati kahawa ulikunywa mchana au asubuhi.
Chokoleti nyeusi.
CHOKOLETI NYEUSI (Dark chocolate)
Ingawa
chokoleti kwa kawaida, huwa na faida ya kuimarisha kinga ya mwili kwa
kuwa na kiasi kingi cha virutubisho aina ya ‘antioxidant’, lakini pia
ina kiwango kingi cha ‘caffeine’ ambacho kinaweza kuchangia ukosefu wa
usingizi kama tayari unalo tatizo hilo.
VYAKULA VYENYE VIUNGO VINGI
Vyakula
vilivyoungwa kwa viungo vingi vya aina mbalimbali, zikiwemo pilipili,
huchangia tatizo la chakula kushindwa kusagika vizuri tumboni hali
ambayo humfanya mtu kupata usingizi kwa tabu. Inaelezwa kuwa kirutubisho
aina ya ‘capsaicin’ kinachopatikana ndani ya pilipili, huongeza joto la
mwili na ndicho kinachochangia mtu kukosa usingizi.
VYAKULA VYENYE MAFUTA
Ulaji wa
vyakula vyenye mafuta mengi pia navyo vinatajwa kuchangia ukosefu wa
usingizi au usingizi wa kukatika mara kwa mara. Hivyo katika
kushughulikia tatizo la kukosa usingizi usiku, huna budi kujiepusha na
ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, hasa vile vya kukaanga, muda mfupi
kabla ya kupanda kitandani kulala.
USITUMIE VIDONGE
Wengi
wenye matatizo ya kukosa usingizi hukimbilia kumeza vidonge vya
usingizi. Kitendo cha kumeza vidonge vya usingizi huwa hakiondoi tatizo,
bali husogeza mbele tatizo kwa kuudanganya ubongo. Zaidi wanaotumia
vidonge ili kupata usingizi, huamka wakiwa wamelewa.
DONDOO ZA KUKUSAIDIA KUPATA USINGIZI
Kabla ya
kulala, kunywa glasi ya maziwa moto au ya uvuguvugu. Au kula karanga au
siagi ya karanga (peanut butter). Au kula zabibu kadhaa. Vyakula hivyo,
ingawa vipo na vingine vingi, vinatajwa kuwa na virutubisho
vinavyozalisha homoni za usingizi kwa wingi.
Aidha,
kwa wenye matatizo ya kukosa usingizi kwa muda mrefu, wanashauriwa
kulala kwenye chumba chenye giza kabisa, kujiepusha na kuangalia TV
wakiwa wamelala kitandani, kulala mbali na simu, redio, saa na vitu
vingine vyenye sumaku. Vitu hivi vimeonekana kuharibu mtiririko wa
usingizi kwa njia moja au nyingine hivyo kwa mtu mwenye matatizo ya
kukosa usingizi akaenavyo mbali.