Wanasayansi nchini Marekani
wanasema watu waliowahi kupata maradhi ya moyo wanaweza kuishi maisha
marefu iwapo watakula zaidi vyakula ambavyo havijapitia viwandani.
Watafiti walichunguza zaidi ya watu elfu nne
waliowahi kupata mshituko wa moyo na kubaini kuwa wana uwezekano mkubwa
wa kuishi miaka tisa zaidi kama watakula vyakula hivyo .Vyakula ambayo havijapitia viwandani vina nyuzinyuzi ambazo tayari imethibitishwa kuwa husaidia katika kuwezesha binadamu kwenda haja bila matatizo.
Vyakula ambayo vina nyuzinyuzi hizo ni kama vile matunda, mboga na nafaka.
Hatahivyo wataalam wanasema watu katika mataifa mengi hawali vyakula hivyo kwa wingi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni