HAYA unaweza kuyaita ni maajabu ya mafuta ya samaki baada ya kuonesha
uwezo wa kuponya hata ‘mfu’ aliyekwisha tangaziwa kifo na madaktari
bingwa. Ni kisa cha kweli kilichotokea nchini Marekani hivi karibuni na
kuoneshwa na Kituo cha Televisheni cha CNN ambacho kinaaminika na kutizamwa na mamilioni ya watu duniani.
Septemba 16, 2012 kijana mwenye umri wa miaka 16, Grant Virgin wa nchini Marekani aligongwa na gari
na kuumia vibaya kiasi cha kupoteza fahamu na kuonekana hawezi tena
kupona kutokana na majeraha aliyoyapata mwilini na hasa sehemu ya
kichwa.
Madaktari walijitahidi kadiri ya
uwezo wao kuokoa maisha yake, walifanikiwa kwa kiasi fulani, lakini
kutokana na hali aliyokuwa nayo, waliwatangazia wazazi wake kuwa mtoto
wao hatapona, labda angeweza kuishi kwa usiku mmoja tu.
Wiki mbili baada ya ajali hiyo, kijana Grant alikuwa bado amelazwa hospitalini hajitambui (in a coma) huku familia yake ikielezwa na madaktari kuwa hakuna wanachoweza kufanya zaidi ya kusubiri siku yake ya kufa ifike.
Grant Virgin.
Hata hivyo, wazazi wa Grant hawakukubaliana na maelezo ya madaktari,
badala yake wakaanza kutafuta tiba mbadala kwa kujaribu kufanya kila
aina ya ushauri waliopewa. Walijaribu tiba mbadala tofauti ambazo
zilianza kuonesha matumaini kwa Grant kupata fahamu na kuanza kuongea
maneno mafupi japo kwa taabu.
Wakati wakijaribu tiba hizo mbalimbali, siku moja mama
yake Grant aliona habari moja CNN ikizungumzia uwezo wa mafuta ya
samaki (Omega-3) katika kutibu uvimbe kichwani ambapo ilielezwa namna
ambavyo mafuta hayo yanavyoweza kupunguza au kuzuia uvimbe kichwani.
Ingawa kulikuwa hakuna utafiti mkubwa wa kisayansi wa moja kwa moja
unaoweza kuthibitisha hilo, lakini wazazi wa Grant walianza kumlisha
mtoto wao kwa njia ya mrija mafuta ya samaki kiasi cha gramu 20 kwa
siku. Siku mbili baadaye, kwa mshangao wa kila mtu, Grant akiwa
kitandani hospitali, aliweza kumpigia simu mama yake na kuongea naye kwa
kutamka sentesi kamili.
Awali alikuwa hawezi kuongea kwa sentesi kamili, alikuwa akiongea kwa
taabu na kwa kukatisha na kurudia maneno, (nafikiri unajua mtu
aliyepooza mdomo anavyoongea), lakini baada ya kutumia mafuta hayo kwa
siku mbili tu aliweza kuongea kwa ufasaha, kiasi cha mama mtu kuona kama
ni ndoto.
Aliendelea na dozi ya mafuta ya samaki na kila baada ya muda hali yake
ikawa inaendelea kuimarika, alikuwa hawezi kukaa akaanza kukaa, alikuwa
hawezi kusimama akaanza kusimama, alikuwa hawezi kutembea akaanza
kutembea.
Hivi sasa, mwaka mmoja baadaye, ameweza kupona kabisa huku akifanya
shughuli zake zote, ikiwa pamoja na kucheza michezo mbalimbali na
kusababisha wataalam wa masuala ya tiba kufanya utafiti tena wa kina juu
ya uwezo wa mafuta ya samaki ambayo siyo tu yanasaidia matatizo ya
uvimbe kichwani, bali kwa mwili mzima.
Chanzo kizuri cha kirutubisho aina ya Omega 3 Fatty Acids
ni samaki, hivyo watu wanashauriwa kula samaki. Hata hivyo, kutokana na
uchafuzi wa mazingira, samaki wengi wameharibika na kukosa kirutubisho
hicho muhimu.
Kwa kuzingatia hilo, inashauriwa watu kupata mafuta ya samaki kwa njia
ya vidonge (food suplements) vinavyotengenezwa na makampuni
yanayoaminika kimataifa katika utengenezaji wa bidhaa za vyakula kwa
njia ya vidonge vyenye ubora wa hali ya juu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni