MTU ANAWEZA KUPUNGUZA
UZITO KIASI GANI KWA WIKI?
Mtu anaweza kupungua kilo ngapi kwa wiki ni swali ambalo watu
wengi hujiuliza.Hasa pale wanapotaka kuanza harakati za kupunguza uzito. Ni
wazi kwamba watu wengi hupenda kufanya Diet za muda mfupi na wapate matokea
makubwa ya haraka. (umeula wa chuya, umeutengeneza huo uzito miaka mingapi
unataka upungue kwa dakika ngapi?)
Kiasi cha uzito unaoweza kupunguza kwa wiki hutofautiana kati ya
mtu na mtu. Ingawa nia na juhudi binafsi
huchukua nafasi kubwa katika hili, kuna mambo mengine yanayoleta tofauti
hizo;
1. Jinsi
2. Umri
3. Ukubwa wa mwili
4. Vyakula unavyokula
5. Mazoezi unayofanya
Nguvu joto za chakula (kalori)
Nguvu za chakula yaani kalori, (calories) ni kiasi cha nguvu
ambacho hupatikana au hutolewa na chakula kifikapo mwilini. vyakula vyote vinaidadi fulani ya kalori isipokua maji tu
ambayo hayana kalori.
Kalori hufanya kazi mwilini kama ambavyo mafuta aina ya petroli
au dizeli hufanya kazi kwenye gari. Ili gari iweze kutembea lazima mafuta
yaungue ili kutoa nguvu ambayo hutumika kutembeza gari,na jinsi unavyozidi
kutembea ndivyo ambavyo mafuta huzidi kuungua hadi kwisha.
Mwili wa binadamu nao hufanya hivyo hivyo, nguvu unazopata
kwenye chakula yaani kalori, huungua ili kutoa nguvu ambayo inauwezesha mwili
wako kufanya mambo mbalimbali kuanzia kupumua, kutembea, kukimbia,na yote
ambayo mwiili hufanya. Kadiri
unavyofanya shughuli nyingi zitumiazo nguvu ndivyo ambavyo kalori hupungua
mwilini.
Nusu kilo ( 1/2 kg) ni sawa na kalori
3500. Ili upunguze nusu kilo katika uzito
wako nilazima utoe kalori 3500 katika mwili wako. Unaweza kutoa kalori
hizo katika mwili wako kwa kupunguza kiasi cha kalori unazokula kwa siku
au kwa kuongeza mazoezi au kufanya kazi zinazofanya utumie nguvu nyingi ili
utumie nguvu za ziada ambazo mwili wako umetunza (unene wako)
Kupunguza kalori (chakula) ni muhimu zaidi kuliko kufanya
mazoezi hasa kwa mtu mwenye nia ya kupunguza uzito. Pia mtu anayepunguza uzito haraka zaidi
endapo atapunguza kiasi cha kalori anazokula na kufanya mazoezi ya mwili ili
kuunguza kalori ambazo mwili wake umetunza.
TOFAUTI
Jinsi
ya mtu huchangia katika kuamua ni kiasi gani cha uzito anaweza kupunguza kwa
wiki. Kwa kawaida wanaume wanamisuli mingi kuliko wanawake. Utafiti unaonesha
kwamba misuli hutumia kalori nyingi hivyo uwepo wake katika mwili hufanya mtu
aweze kupunguza uzito haraka. Hii hufanya wanaume waweze kupunguza mwili kwa
haraka kuliko wanawake.
Pia tafiti hizo huonyesha kwamba mtu mwenye uzito mkubwa ana uwezo
wa kupunguza uzito kwa haraka zaidi kuliko mtu mwenye uzito mdogo, hasa
mwanzoni anapoanza kupungua.
MAZOEZI
Kiasi
cha kalori unachoweza kutoa mwilini unapofanya zoezi au shughuli nyingine
hutokana na uzito wa mtu. Mtu mwenye uzito mdogo hutoa kalori chache na mwenye
uzito mkubwa hutoa kalori nyingi kwa kiasi kilekile cha mazoezi.
Mfano:mtu mwenye kilo 72.5 atatoa calories 986 kwa kukimbia kwa
dakika 60, lakini mwenye kilo 108 atatoa calories 1,472 kwa kukimbia dakika
hizohizo 60
Kadiri unavyotoa kalori nyingi mwilini ndivyo uzito unavyozidi
kupungua
DIET
Diet kali hulenga kumfanya mtu apunguze uzito mwingi ndani ya
muda mfupi. Tafiti huonyesha kwamba asilimia kubwa ya uzito unaopotea
unapofanya diet kali ni uzito wa maji mwilini.
Ni ngumu sana kwa mwili kutoa kilo 1 ya mafuta mwilini kwa
wiki. Hata hivyo endapo utaendelea na
diet kali kwa muda mrefu basi unaweza kupunguza mafuta ya mwili na hivyo
kupunguza mwili kwa haraka.
Ukifanya diet kali sana ,ambayo inakufanya uingize kalori chache
sana mwilini basi kuna uwezekano wa kupunguza kilo ndani ya muda mfupi.
MAGONJWA NA MATIBABU
Historia ya afya yako ni Sababu nyingine inayochangia katika
kujua kiasi cha kilo unachoweza kupunguza kwa wiki. Magojwa yasababishwayo na homoni za mwili
hufanya iwe ngumu sana kupunguza uzito wa mwili.
Tafiti zinaonyesha kwamba baadhi ya madawa kama madawa ya
kisukari na dawa za uzazi wa mpango hufanya iwe ngumu kupunguza uzito. Baadhi
ya madawa pia hufanya mtu ashindwe kabisa kupunguza uzito na madawa mengine
hunenepesha mwili.
USHAURI
Endapo umekua ukifanya mazoezi na diet kwa muda mrefu na
hupungui uzito, ni vyema ukamuaona Daktari wako na kumuelezea hali hiyo ili
aweze kutafuta chanzo cha tatizo hilo na kulitafutia ufumbuzi.
Kama unafanya juhudi za kupunguza uzito basi punguza kiasi cha
kalori unazokula kwa siku na pia fanya mazoezi ili kuunguza kalori za akiba
mwilini.
HITIMISHO.
Naamini umeelewa nikwanini hakuna kipimo maalumu cha kiasi cha
uzito ambao mtu anaweza kupunguza kwa wiki, kwani vigezo vyote hivi huchangia
katika kupungua.
Hata ivyo vitu kama msongo wa mawazo na kutokupata usingizi
wakutosha, pia huweza kuchangia mtu kupungua uzito au kuongeza uzito.
Huna sababu za kutumia madawa ...na buberwa Robert blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni