mapishimapishi

mapishimapishi

Jumapili, 15 Septemba 2013

JIFUNZE KUTENGENEZA MAPISHI HAYA TOKA KWA CHEF ANNA LUSINDE NA CHEF AZIZA JAFARI


 
JIFUNZE KUTENGENEZA JUISI HII YA MCHANGANYIKO WA MATUNDA KUTOKA KWA CHEF ANNA LUSINDE
 
MAHITAJI
 
1pc parachichi
3pc tunda pasheni
1 pc embe
1 pc karoti
 
FATILIA PICHA NA MAELEZO CHINI JINSI YA KUANDAA
 
 
menya matunda yote pamoja na karoti kama muonekano katika picha

 
Kisha weka katika blenda na usage

 
Saga wastani kwa spidi ya kawaida kisha chuja hakikisha mbegu zisisagike

 
Chuja kwa chujio pole pole

 
Huu ni muonekano wa jusi baada ya kuchujwa

 
Pata juisi hii pamoja na chakula kumbuka mchanganyiko wa matunda hayo unasukari ya kutosha waandalie familia wafurahie
 
 
JIFUNZE KUTENGENEZA VIAZI MCHANGANYIKO WA MBOGA NA SAUSAGE TOKA KWA CHEF AZIZA JAFARY
 
MAHITAJI
 
1 kg viazi ulaya
5 pc sausage
2 pc pili pili hoho
2 pc carrots
2 pc vitunguu maji
4pc kitunguu swaumu kidogo na bizari nyembamba, mafuta kidogo na chumvi basi
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
 
chemsha viazi kwa maji na chumvi tu usiweke mafuta

 
weka mafuta katika kikaango acha ipate moto kisha weka mchanganyiko wa mboga zote pamoja na sausage endelea kukaanga utapata harufu safi sana

 
Kisha chukua mchanganyiko wa sausage na umwagie juu ya viazi, chef Aziza Jafary alikunywa koka pamoja na chakula hiki safi sana kwa afya ya mlaji.
kwa msaada wa active chef
 
 

JIFUNZE KUPIKA PASTA NA NYAMA YA KUSAGA ( MEAT BALLS)


KAA TAYARI UJIFUNZE KUTENGENEZA PASTA NA MEAT BALLS PAMOJA NA MCHANGANYIKO WA MBOGA MAJANI KWA NJIA YA VIDEO


Huu ni muonekano wa maandalizi ya vitu vya kupika pasta, spinach na meat balls
 kwa msaada wa activechef

JIFUNZE KUPIKA NYAMA YA MBUZI NA VIAZI ULAYA VYAKUOKA KATIKA OVEN



CHINI KABISA MWISHO WA BLOG ANGALIA RECIPE YA KEKI IPO TAYARI
JIFUNZE KUPIKA CHAKULA HIKI KITAMUA NA RAHISI SANA KWA MCHANGANYIKO WA MBOGA MAJANI, NYAMA YA MBUZI NA VIAZI ULAYA KWA MTINDO HUU WA MAPISHI UNAWEZA PIKA NYAMA YA KUKU, SAMAKI AU NYAMA YA NG,OMBE
MAHITAJI
JINSI YA KUANDAA FATILIA VIDEO YA MAFUNZO HAPO CHINI

Huu ni muonekano wa picha ya vyakula kwaajili ya maandalizi

Huu ni muonekano wa picha ya chakula kimeshaiva baada ya kutoka
 

JIFUNZE KUTENGENEZA KITAFUNWA CHA DENGU



KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA MUDA SI MREFU

MAHITAJI

250 gram dengu kavu au Chickpeas,
1 kijiko kidogo cha chai mafuta ya kupikia
1 Bay Leaf sio lazima ni kwajili ya harufu
1/2 kijiko kidogo cha chai mchanganyiko wa unga wa Cumin na Coriander
1/2 kijiko kidogo cha chai Pili pili nyekundu ya unga
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
Muda wa maandalizi : Masaa 4 hadi 8
Muda wa mapishi : Dakika 30 hadi saa 1
Idadi ya walaji : Watu 4
Baada ya kuiva ujazo : 500 gram
 
 
 
  kwa msaada wa activechef blog

JIFUNZE JINSI YA KUPIKA MKATE HUU MWEUPE


JIFUNZE KUTENGENEZA MKATE HUU MWEUPE NI RAHISI NA NAFUU KUANDAA ONYESHA UJUZI WAKO KATIKA FAMILIA
 
MAHITAJI
 
1 kg unga wa ngano
2 kijiko kidogo cha chai chumvi
240 gram maziwa ya maji ya vugu vungu
60 gram maji ya vugu vugu
2 kijiko kikubwa cha chakula siagi, iyeyushe
3 kijiko kikubwa cha chakula asali
2 kijiko kidogo cha chai amira ya chenga

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
Muda wa maandalizi : Masaa 2 hadi 4
Muda wa mapishi : Dakika 30 hadi saa 1
Idadi ya walaji : Watu 4
Ujazo : Unapata mkate wenye 9-inch
 
 
Chukua robo tatu ya unga pamoja na chumvi kisha chukua mchapo na uchanganye. 

 
 Chukua bakuli safi kavu kisha changanya maziwa, majina, siagi, chumvi pamoja na amira. Hakikisha joto la maziwa na maji liwe 110 degrees.

 
 Mimina mchanganiko wako wenye maziwa katika unga.

 
Anza kukanda pole pole 

 
Hapa mchanganyiko wako umeshaanza kushikana. 

 
Chukua mchanganyiko wako kisha weka juu ya meza hakikisha umemwagia unga kwa juu endelea kukanda vizuri kwa dakika 10.

 
Kama unafikiri mchanganyiko bado una maji maji, basi chukua robo ya unga iliobakia tumia kijiko kikubwa cha chakula ongeza kimoja kimoja epuka kuweka unga wote ukazidisha.

 
Chukua bakuli safi na kavu, kisha lipake mafuta na weka mchanganyiko wako katika hiyo bakuli. 

 
KIsha tumia plastic na funika weka sehemu yenye joto, jikoni kuna joto.

 
Hakikisha mchanganyiko wako umeongezeka mara 2, ndani ya dakika 40 mpaka 50. 

 
Kisha chukua mchanganyiko wako ukande vizuri na weka katika chombo chako cha kuokea kiwe cha chuma au cha kioo kama changu chenye ukubwa wa  8.5 X 4.5 X 2.5 (1.5 Lita).

 
 Kisha funika tena kwa plastic

 
 Weka pembeni kwa dakika 20 mpaka 30 itakua imeshaumuka vizuri kama unavyoona katika picha weka katika oven.

 
 Kumbuka oven yako unatakiwa uiwashe kabla katika joto la 350 degrees, ukishaweka unga katika oven unaweza rushia maji kidogo ili kuweka mvuke utakao saidia kuweka rangi nzuri ya brown na kua na gamba gumu. Oka kwa dakika 40 mpaka 50 mkate wako utakua umeiva.

 
Toa mkate wako katika pan, hamishia katika wire rack, ili mkate uweze kupoa.

 
Kata kata vipande na wapatie walaji, unaona mkate ulivyochambuka. 

 
Unaweza ukavuta picha huu mkate ni mtamu kiasi gani ukishapaka siagi kwajuu? au ukipaka jam pia? Ni mtamu sana sana.
  kwa msaada wa activechef blog

JIFUNZE KUPIKA YA MUFFIN YENYE MCHANGANYIKO WA VIPANDE VYA CHOCOLATE NA KARANGA


 
RECIPE SAFI KABISA YA MUFFIN YENYE MCHANGANYIKO WA VIPANDE VYA CHOCOLATE NA KARANGA NI TAMU RAHISI NA NI NAFUU KUANDAA

MAHITAJI

250 gram siagi laini
250 sukari
2 mayai
250 gram plain yogurt
1 kijiko kidogo cha chai vanilla
500 gram  unga wa ngano
1 kijiko kidogo cha chai baking soda
1/2 kijiko kidogo cha chai baking powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
180 gram vipande vya chocolate
1 kijiko kidogo cha chai cinnamon powder
4 kijiko kikubwa cha chakula karanga za kuoka
2 kijiko kikubwa cha chakula sukari ya brown
60  gram vipande vya chocolate
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
Muda wa maandalizi : Dakika 30
Muda wa mapishi : Dakika 30
Idadi ya keki : 12 Muffins
 
Katika bakuli changanya sukari na siagi pamoja.
 
Kisha mimina mayai pole pole endelea kuchanganya katika mchanganyiko wa sukari na siagi.
 
Kisha ongeza yogurt na vanilla na uchanganye ichanganyike vizuri.
 
Kisha chukua bakuli safi na uchanganye unga wa ngano pamoja na baking soda, baking powder na chumvi.
 
Kisha chukua mchanganyiko wa unga kisha mimina polepole katika mchanganyiko wa mayai.
 
Kisha mimina vipande vya chocolate na uendelee kuchanganya polepole.
 
KIsha chukua tray ya kuokea na weka vikombe vya karatai kisha mimina mchanganyiko wako 2/3 hakikisha isijae kabisa.
 
Kisha chukua bakuli kavu weka vipande vya chocolate vilivyobakia, cinnamon powder na karanga changanya pamoja.
 
Kisha mwagia kwa juu mchanganyiko huo kwenye tray ya kuokea izibe ile nafasi iliyobakia.
 
Hakikisha oven unaiwasha dakika 5 kabla ya kuoka Choma katika ovena katika moto wa 350F kwadakika 20 had 30. Poza keki zako kwa dakika 5 kabla ya kuzitoa katika pan.
 
Naimani ukizieweka sehemu nzuri ukafunika safi zisiguswe na wadudu zinaweza kukaa kwa siku tatu bila ya kuharibika!
 
 WAANDALIE FAMILIA AU WATEJA WAKO WAFURAHIE.
  kwa msaada wa activechef blog