NI RAHISI, NAFUU NA HARAKA SANA KUANDAA 
AINA HII YA MAPISHI YA SAMAKI KWA KUTUMIA FOIL NA KUOKA KATIKA OVEN 
LAKINI SAMAKI ATATOKA KAMA AMECHEMSHWA NA AKIWA NA LADHA SAFI SANA BILA 
YA KUPOTEZA VIRUTUBISHO VYOTE MUHIMU.
MAHITAJI
1pc kitunguu maji kikubwa
1 pc limao kubwa
5 gram binzali
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
1 pc pili pili hoho kubwa
50 gram tomato pest ( nyanya ya kopo)
kipande cha foil kutokana na ukubwa wa samaki
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Huu ni muonekano wa samaki akiwa mbichi tayari umeshamsafisha vizuri kwa
 maji baridi na mapishi haya unaweza tumia kwa samaki aina ya sato, 
sangara, kibua, change, jodari au kole kole na akaiva na ladha safi 
kabisa.
Katika picha unaona mchanganyiko wa vitunguu, pilipili hoho, maji ya 
limao, binzali, chumvi, pili pili manga na nyanya ya kopo baada ya 
kuchanganya pamoja kasha mpakae samaki pande zote mbili ulizompasua ili 
mchanganyiko huu uingie vizuri katika nyama kasha mabaki ya huo 
mchanganyiko mjazie tumboni kisha mfunike vizuri na foil muweke katika 
oven tayari ikiwa na moto.
Jana mchana niliporudi nyumbani niliandalia samaki aina ya sato pamoja 
na maharage ya Nazi na ugali wa mahindi nipo ulaya lakini na kula 
chakula nilichokizoea nyumbani Tanzania na kwa ladha na ubora ule ule.
Unaweza kumpika katika oven kwa dakika 30 kwenye moto wa degree 200 hadi
 250 pia kwa mtindo huu unaweza kumchoma katika jiko la mkaa akiwa hivi 
hivi katika foil na akaiva safi kabisa
Baada ya nusu saa samaki wako atakua ameiva na atakua na muonekano kama huu na ladha safi sana
Hapa sasa ndio nilikua namfunua vizuri tayari kwa chakula cha mchana
Hata kama samaki amekaa kwenye friza kwa muda mrefu mchanganyiko huu wa 
mboga majani limao na viuongo vinasaidia sana kuamsha ladha ya samaki 
wako pika familia ifurahie.
kwa msaada wa activechef 






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni