RECIPE SAFI KABISA YA MUFFIN YENYE MCHANGANYIKO WA VIPANDE VYA CHOCOLATE NA KARANGA NI TAMU RAHISI NA NI NAFUU KUANDAA
MAHITAJI
MAHITAJI
250 gram siagi laini
250 sukari
2 mayai
250 gram plain yogurt
1 kijiko kidogo cha chai vanilla
500 gram unga wa ngano
1 kijiko kidogo cha chai baking soda
1/2 kijiko kidogo cha chai baking powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
180 gram vipande vya chocolate
1 kijiko kidogo cha chai cinnamon powder
4 kijiko kikubwa cha chakula karanga za kuoka
2 kijiko kikubwa cha chakula sukari ya brown
60 gram vipande vya chocolate
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Muda wa maandalizi : Dakika 30
Muda wa mapishi : Dakika 30
Idadi ya keki : 12 Muffins
Katika bakuli changanya sukari na siagi pamoja.
Kisha mimina mayai pole pole endelea kuchanganya katika mchanganyiko wa sukari na siagi.
Kisha ongeza yogurt na vanilla na uchanganye ichanganyike vizuri.
Kisha chukua bakuli safi na uchanganye unga wa ngano pamoja na baking soda, baking powder na chumvi.
Kisha chukua mchanganyiko wa unga kisha mimina polepole katika mchanganyiko wa mayai.
Kisha mimina vipande vya chocolate na uendelee kuchanganya polepole.
KIsha chukua tray ya kuokea na weka vikombe vya karatai kisha mimina mchanganyiko wako 2/3 hakikisha isijae kabisa.
Kisha chukua bakuli kavu weka vipande vya chocolate vilivyobakia, cinnamon powder na karanga changanya pamoja.
Kisha mwagia kwa juu mchanganyiko huo kwenye tray ya kuokea izibe ile nafasi iliyobakia.
Hakikisha oven unaiwasha dakika 5 kabla ya kuoka Choma katika ovena
katika moto wa 350F kwadakika 20 had 30. Poza keki zako kwa dakika 5
kabla ya kuzitoa katika pan.
Naimani ukizieweka sehemu nzuri ukafunika safi zisiguswe na wadudu zinaweza kukaa kwa siku tatu bila ya kuharibika!
WAANDALIE FAMILIA AU WATEJA WAKO WAFURAHIE.
kwa msaada wa activechef blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni