CHAPATI
HIZI NI SAFI KABISA KWA FAMILIA KUBWA KUTOPIKA MARA KWA MARA UNAPIKA
NYINGI NA UNAZITUNZA WIKI MOJA NA ZIKABAKI NA UBORA ULEULE, PIA NYAMA
HII YA MBUZI INAKUA HAINA HARUFU MTU YEYOTE ANAWEZA KULA KWA AINA HII YA
MAPISHI NA AKAFURAHIA SANA
MAHITAJI
1 kg unga wa ngano
1 kikombe kimoja
1 kijiko kidogo cha chai chumvi
nusu kikombeha chai mafuta ya kupikia
2 mayai kuongeza ladha
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEKEZO CHINI
unga wa ngano
Weka mafuta katika unga
kisha weka moto sana katika unga
kisha changanya kwa kutumia mwiko maana maji ni yamoto sana
weka chumvi
kishaanza kukanda kwa mkono maji yatakua yameshapoa
kanda unga safi kabisa uchanganyike
kisha anza kusukuma unga wote
baad ya hapo mwagia kwa juu mafuta ya kula pakaza eneo lote
hakikisha mafuta yameenea unga wote
kisha kunja pole pole unga wote kutengeneza mduara
kisha kata maumbo madogo ya usawa kwa kutumia kisu
baada ya hapo chuku yale maumbo uliyokata geuza na uyakandamize safi mpka chini
hapa ni baada ya kuzikandamiza
kisha chukua mti wa kusukumia na zisukume mapak upate upana wa kawaida tayari kwa kuzichoma
weka katika kikaango kikavu kisha zungusha chapati hiyo kw kutumia mkono
iache kidogo ichomwe
kisha igeuze baada ya kuiva upande mmoja
ikandamize tena kwa upande wa pili bado ikiwa kavu bila mafuta kama ni yamoto sana basi tumia karatasi kukandamizia
weka mafuta ya kupikia kwa juu hakikisha unasambaza chapati yote ienee
kisha geuza a upande wa pili paka pia mafuta
Toa weka katika sahani itakua imeiva safi kabisa tayari wa kuliwa
weka
pembeni zipoe kisha unaziwekakatika sahani unatumbukiza katik mfuko wa
plastiki usiweke kwenye friji weka tu nje zitakua safi na laini zinakaa
wiki 1 baada ya hapo zitapoteza ubora ukitaka kula unatoa unapasha
kwenye kikaango au kwenye micro wave inakua yamoto na laini zaidi na
iliyochambuka kwa ubora uleule
MAHITAJI NYAMA YA MBUZI
1 kilo nyama ya mbuzi
1 kitunguu kikubwa
1 nyanya ya kopo
1 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu
3 viazi ulaya
1 kikombe kilichojaa mchanganyiko w mboga majani
1 kikombe cha maji baridi
1/2 kikombe mafuta ya kupikia
weka mafuta katika sufuri yakishapata moto weka kitunguu maji kaanga
hii ni nyama ya mbuzi ya mifupa inaladha yake ya kipekee sana
kaanaga
vitunguu mpaka viwe vya kahawia ili kuleta ladha nzuri katika mchuzi
wako na kuondoa harufu ya mbuzi ili mtu yeyote yule aweze kula
baada ya kitunguu kuwa kahawia weka nyama ya mbuzi piaendkea kukaanga
ongeza maji kiasi ili sufuria isiungue pamoja na nyama
kisha weka chumvi
acha mbuzi ichemke na itakua na mchuzi wa kahawia
kisha weka kitunguu swaumu hicho ni kifaa maalumu cha kusagia kitunguu swumu
baada yahapo weka viazi uklaya vilivyomenywa safi na kukatwa katwa vidogo
kisha weka nyanya ya kopo
kisha weka mchanganyiko wa mboga majani ( caroti, njegere na pili pili hoho, mahindi machanga ya njano)
kuongeza ladha zaidi unaweza weka unga wa binzali au rojo la binzali
MAFUNZO SAFI KABISA YA CHAPATI NA NYAMA YA MBUZI WAPIKIE FAMILIA YAKO CHAKULA BORA NA SALAMA WAFURAHIE.CHANZO ACTIVE CHEF
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni