KAA TAYARI KWA KUJIFUNZA JINSI YA KUKAANGA YAI KWA KUCHANGANYA NA CHEESE
MAHITAJI
2 pc yai vunja tenga ute mweupe tu
1 pc yai Zima usilitenganishe
2 kijiko kidogo cha chai maji safi
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
60 gram Gruyere Cheese au Cheddar cheese
1 fungu Chives
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Vunja mayai 2 kwenye bakuli safi hakikisha unaweka ute mweupe tu kasha
vunja yai moja Zima mwagia katika bakuli ulilitenganishe kasha weka
chumvi na pili pili manga. Tumia mchapo kupiga piga ichanganyike
Kisha weka maji safi au unaweza tumia maziwa badala ya maji. Ukitaka yai lako liwe fluffier au spongy basi tumia maji.
Hutakiwi kupiga piga sana maana utasababisha mapovu kama unavyoona
kwenye picha hii haitakiwi. pia unaweza kutumia uma kwenye kupiga piga
na mchanganyiko wako ukawa safi. Unaweza kuweka hebs ya aina upendayo
mfano parsley au korienda au chives
Weka kikaango katika moto kwa muda kiasi ipate moto. Kisha mwagia siagi
ukiona imeaanza foaming and sizzling basi moto up safi. Tumia vijiko
viwili vidogo vya chai siagi kasha mwagia mchanganyiko wako wa yai
kwenye kikaango.
Kumbuka kulivuruga vuruga yai kwa sekunde 6 hadi8 ili liweze kuiva haraka upande wa chini
Kisha lisambaze vizuri na uliache liweze kuiva
Baada ya dakika chahe utaona yai lote mieshakauta ute na kua na muonekano kama kwenye picha Zima jiko.
Mwagia cheese kwa kufata mstari kati kati ya yai kama muonekano katika picha. Kumbuka usimwagie kwenye yai lote.
Chukua upande wa kwanza funika yai lako kisha chukua upande wa pili na ufunike pia na kupata umbo lionekanalo katika picha.
Ukilikata yai lako baada ya kuiva utaona cheese inamwagika ooooh safi sana. See that cheese oozing out from the middle?
Unaweza ongeza ladha ya yai kwa kuweka vilivyotajwa hapo chini
Crumbled Goat Cheese, sautéed shallots and fresh(or dried) thyme
Grated Emmentaler, sautéed Mushrooms and Spinach
Caramelized Onions, Crisped cubed Tempeh and fresh Marjoram
Grated Gouda and lightly stir fried thinly sliced (on the diagonal) Asparagus
Maji: Sio lazima kutumia maji unaweza tumia maziwa na
utumiaji maziwa unasababisha creamier texture wakati ukitumia maji
inasaidia fluffiness kwenye yai.CREDIT ACTIVE CHEF
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni