MAANDAZI
HAYA YANALADHA SAFI SANA KWA MLAJI NI RUKSA KUONGEZA KIUNGO AU
KUPUNGUZA NA ANDAZI LAKO LITABAKI NA UBORA ULE ULE MAANA SIO WATU WOTE
WANAPENDA VIUNGO.
MAHITAJI
1 kikombe cha chai kikubwa
2 Amira ya chenga kijiko kidogo cha chai
1 kilo unga wa ngano
1 hiriki kijiko kikubwa cha chakula
1 kikombe cha chai tui zito la nazi na vijiko viwili vya mafuta ya kupikia ya baridi (1 kikombe cha chai mafuta ya moto kamahutumii tui la nazi )
1 chumvi kijiko kidogo cha chai
1 maji ya moto wa wastani kikombe kikubwa cha chai
Hii ni hiriki , sukari na Amira ya chenga
Weka sukari, Amira, chumvi na hiriki katika bakuli kisha weka mafuta yakupikia vijiko viwili
kisha weka tui la nazi
Kisha changanya unga wa ngano kilo moja katika bakuli
kisha weka maji ya moto katika unga
Anza kukanda unga
Kisha sukuma unga mpaka upate unene wa saizi ya andazi unalotaka
Kisha kata andazi kwa saizi ya andazi la ukubwa unaotaka
Haya ndio maandazi mabichi baada ya kukatwa tayari kwa kuchomwa acha yaumuke kwa dakika 10 ili utakapochoma yasijae mafuta ndani
Weka mafuta ya kupikia katika kikaango kisha yapate moto wa wastani yasiwe yamoto sana maandazi yakaungua pia hayataiva ndani
HUU
NDIO MUONEKANO SAFI WA MAANDAZI YA HIRIKI NA TUI LA NAZI ENJOY NA
FAMILIA YAKO KWA CHAI YA JIONI AU CHAI YA ASUBUHI KWA KITAFUNWA SAFI NA
SALAMA MAANA HAKINA MAFUTA MENGI PIA CHUMVI INAAIDIA KUKIMBIZA MAFUTA
KATIKA UNGA.CHANZO ACTIVE CHEF
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni