mapishimapishi

mapishimapishi

Jumatano, 29 Januari 2014

TASTE OF TANZANIA: MODERN SWAHILI RECIPIES FOR THE WEST BY MIRIAM R. KINUNDA.


This cookbook brings a unique perspective to East African and Swahili cooking. It is a colorful, well arranged book that combines a simple step by step method for arriving at delicious dishes of the East African region. This book is by far the most comprehensive compilation of Swahili recipes presented in a contemporary appealing format.

This one of a kind and interesting book compiles and explains the cuisine of the well-known Swahili culture, which spans over six Africans countries including Tanzania, Kenya, Congo, Rwanda, Swahili and Burundi. A fascinating thing this book does is to explore the interconnectedness of humanity through food. Arab and Indian influences on Swahili cuisine are mentioned and thus enriching our knowledge as well raising new questions that beg for further academic inquiries.

Thus many people around the world think Swahili is a Language, this book would allow people to see that Swahili is also a culture of delicious and simple recipes that calls for fresh ingredients.
The recipes inside calls for freshest ingredients thus suit every person regardless religion, age vegetarian, people who choose to eat organic food.
a.     Organic food lovers can have a choice of buying their ingredients from organic food stores
b.     Vegetarians will find this book useful in expanding the choice of food we eat; lot of vegetarian recipes.
c.     Sweets and snacks for the little ones to enjoy.
d.     Muslims will enjoy the book, they do not have to worry about Halal ingredients since all recipes call for fresh ingredients, and thus they have a choice on where to buy their ingredients. There is only one recipes call for pork; which can be skipped.



In a few months, this book will be available at your favorite bookstores in Tanzania, Europe and other countries. Visit TasteofTanzania.com for a follow up.

U can also visit her YouTube channel Taste of Tanzania

Alhamisi, 23 Januari 2014

UREMBO: Punguza kilo tano kwa siku saba

fat thin fitness thumb1 3eb1d
NI wanawake wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri.
Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha maradhi mbalimbali bali pia mwonekano wako unakuwa si mzuri. Zifuatazo ni njia za kupunguza unene ndani ya siku saba.(HM)
Siku ya 1: Asubuhi kula matunda (lakini usile ndizi). Mchana chemsha kabichi, weka chumvi kidogo na nyanya, chemsha na upate supu. Kula mchanganyiko huo na utajiona umeshiba. Jioni kula tikiti maji na mbogamboga au kabichi uliyotengeneza mchana.
Siku ya 2: Kula mboga za majani asubuhi (usile mboga za majani zenye wanga kama karoti). Mchana kula kabichi iliyochemshwa, tengeneza na kachumbari. Katika kabichi weka chumvi, pilipili na mafuta ya olive. Jioni unaweza kula mlo kama wa mchana lakini unaweza kukaanga mboga nyingine za majani.
Siku ya 3: Kula mboga za majani na matunda, unaweza kuongeza kiazi kitamu kimoja.
Siku ya nne 4: Kula ndizi moja na unywe na maziwa ya mtindi
wakati wa asubuhi. Mchana kula kabichi kama ulivyoitengeneza kwenye siku ya kwanza, usiku rudia mlo wa mchana.

Siku ya 5: Kula nyanya nne pamoja na samaki au kipande cha kuku asubuhi. Mchana unaweza kula samaki wa kuchemsha kiasi ambaye amechanganywa na nyanya. Wakati wa jioni unaweza kula chakula kama cha mchana.
Siku ya 6: Unaweza kula chakula cha protini na mboga za majani. Anza kwa kula kachumbari asubuhi. Mchana kula tambi kiasi na kipande kidogo cha samaki
. Usiku tengeneza supu ya kabichi.

Siku ya 7: Anza kwa matunda na juisi. Mchana kula mboga za majani na usiku kula supu ya kabichi na kiazi kimoja.
Kumbuka: Unatakiwa kunywa maji angalau glasi nne kila siku. Usiendelee kwa muda mrefu, kumbuka dayati hii ni ni kwa siku saba. pekee. Chanzo: mwanaspoti

Jumanne, 21 Januari 2014

JIFUNZE KUTENGENEZA KITAFUNWA HIKI CHA KARANGA NA CHOCOLATE




PIA NITAKUPATIA RECIPE SAFI KABISA YA KITAFUNWA HIKI CHA KARANGA NA CHOCOLATE

MAHITAJI

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI













VIJUE VYAKULA BORA NA FAIDA ZAKE MWILINI

TUNAAMBIWA kuwa kuishi vizuri ni pamoja na kula chakula bora na sahihi. Pia, mtu anayeishi vizuri ni yule ambaye hasumbuliwi na maradhi hatari na njia pekee ya kuulinda mwili dhidi ya maradhi hatari ni kujua ipasavyo na kuvitumia vyakula bora pamoja na kufanya mazoezi.

Katika makala yafuatayo, nitakuorodhoshea baadhi ya vyakula vinavyotajwa kuwa bora (super foods) ambavyo faida zake mwilini zimeanishwa. Kwa mlaji, linakuwa jambo la busara kujua faida ya kila chakula unachoingiza tumboni.

Kwa mujibu wa mwandishi wa makala kuhusu vyakula hivi bora, Bw.Hakeem Rahman, hivi ni vyakula vinavyowafanya “wenye afya nzuri kuendelea kuwa na afya nzuri zaidi na wenye afya mbovu, kuwa na afya nzuri.”
SAMAKI
Wana virutubisho aina ya Omega 3 ambavyo huulinda moyo dhidi ya maradhi. Samaki pia wana virutubisho vinavyomuongezea mlaji uwezo wa kukumbuka (memory), kuna virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na kansa mwilini, kuongeza kinga mwilini na kuondoa mafuta mabaya mwilini (Bad cholesterol). (unashauriwa kula samaki kwa wingi kadiri uwezavyo).

Baadhi ya virutubisho muhimu vinavyopatikana kwenye samaki ni pamoja na vitamini D, vitamin 12, Vitamini B3, vitamini B6,  Omega 3 Fatty Acids, Protini na madini mengine mengi.

KAMBA (PRAWNS)
Samaki aina ya kamba hutoa kinga dhidi ya maradhi ya moyo, shinikizo la damu (High Blood Pressure), huboresha ‘mudi’ ya mtu, huondoa mfadhaiko wa akili na hupunguza maumivu ya viungo. (unashauriwa kula kamba japo mara moja kwa wiki.

KARANGA
Unaweza ukazidharau karanga, lakini zina faida kubwa mwilini. Miongoni mwa faida zake ni pamoja na kuimarisha afya ya moyo, hupunguza kolestro mbaya mwilini na kuongeza kolestro nzuri. Mafuta mazuri yaliyomo kwenye karanga hupunguza shinikizo la juu la damu na huponya magonjwa ya moyo na hupunguza uzito. Faida zote hizi unaweza kuzipata kutoka kwenye karanga au siagi iliyotengenezwa kutokana na karanga (peanut butter). (unashauriwa kula kiasi kadhaa kila siku, hasa za kuchemsha ndiyo nzuri).

KAROTI
Miongoni mwa faida nyingi za karoti ni pamoja na kushusha kolestro mbaya mwilini, kupunguza unene, kuimarisha nuru ya macho, kuimarisha shinikizo la damu, inatoa kinga kwenye figo na inaimarisha sukari mwilini. (kula kadiri unavyoweza, mbichi au zilizochemshwa).

MAHARAGE YA SOYA
Haya ni maharage bora kabisa ambayo yana faida nyingi mwilini, ikiwemo kushusha shinikizo la damu, kuimarisha sukari mwilini, kupambana na ugonjwa wa kisukari, figo, moyo, kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa kansa ya kibofu na magonjwa mengine ya wanawake.

PAPAI, TIKITI MAJI
Miongoni mwa matunda muhimu mwilini ambayo hata mgonjwa wa kisukari anashauriwa kuyala ni pamoja na papai na tikitimaji ambayo yanaelezwa kuwa na kiwango kikubwa cha kamba lishe (fibre) na hivyo kutoa mchango mkubwa sana katika kuimarisha kiwango cha sukari mwilini. (kula kiasi cha moja katika ya matunda hayo mawili, kila siku).
Itaendelea wiki ijayo.Chanzo GPL

Alhamisi, 16 Januari 2014

JINSI YA KUPANDA, UMWAGILIAJI, UVUNAJI NA FAIDA YA MATUNDA AINA YA PARACHICHI .


Sehemu ya Kwanza.. 
Kama ada kama dawa blog yetu inajieleza kwamba itakuwa inakumbusha au kutoa elimu ya vitu tunavyovijua lakini tumesahau au hatufuatilii, nah ii yote ni kutaka kukupa changamoto wewe msomaji ili uweze kufikiri njia nyingine ya kuweza kujiongezea kipato kupitia kilimo pia. 

Upandikizaji hujumuisha aina mbili za mimea. Unachukua mmea mmoja ambao unadhani hauna tija nzuri, na sehemu ya mmea mwingine ambao una ubora zaidi na kupandikiza kwa kukata na kufunga pamoja ili kupata mbegu bora zaidi.
 
Kwenye shamba la bwana Buberwa Robert, atakuwa na kitalu chenye zaidi ya miche 1500 ya miparachichi, ikiwa inasubiri kufikia wakati wa kupandikiza. 

Mbinu anayotumia
 
Kukusanya kokwa za parachichi kutoka maeneo ya sokoni; atakachofanya ni kuhakikisha tu kuwa mbegu hiyo ni safi, haijaathiriwa na magonjwa na itaota. Baada ya hapo huchagua zile zenye muundo mzuri na kuzipanda kwenye boksi au kwenye sehemu ya kitalu. Baada ya kuota ataziotesha kwenye makopo, au kwenye viriba kisha kuendelea kumwagilia maji mpaka zinapokuwa na umbo usawa wa penseli. Upandikizaji ni lazima ufanyike wakati mmea umefikisha unene wa penseli. Kupandikiza kwa kutumia chipukizi lililolingana na mche unaopandikizia ni njia yenye mafanikio zaidi.
 
Upandikizaji ni lazima ufanyike wakati ambao mizizi bado ni laini. Pandikizi litakalotumika wakati wa kupandikiza ni lazima lisiwe katika hatua ya ukuaji kwa wakati huo, na ni lazima umbo liwiane na mti linapopandikizwa kuzuia maji yasipotee na kusababisha pandikizi kukauka.

Mapandikizi ni lazima yatokane na aina ya parachichi ambazo zimeboreshwa kama vile HASS, FUERTE  au PUEBLA . Kwa wale wakulima ambao mmea utatoa majani mapya. wana mkataba na Africado, watahitaji kupata mapandikizi kutoka kwenye miti ya HASS. Hii ina maanisha kuwa mkulima anayetaka kuanzisha kitalu kwa ajili ya kupandikiza ni lazima apande walau miti 5 ya parachichi aina ya HASS ili kupata mapandikizi.
 
Njia ya kupandikiza ina ufanisi zaidi na ni rahisi kuliko kupanda miche upya, kwa kupandikiza inagharimu chini ya asilimia 75, kuliko kupanda miche upya na kuweza kupata aina ambayo inastahimili magonjwa. Wakulima pia wamekuwa na rekodi nzuri ya ongezeko la mavuno kutokana na mimea waliyopandikiza, pamoja na upungufu wa matumizi ya madawa.


Wakulima ambao wanafanya kazi zao chini ya CARITAS Njombe sasa wanaona faida kubwa inayotokana na kupandikiza, wameamua kuwekeza kwenye utaalamu huu na kuwa na miche mingi kwenye vitalu vyao. Hii ni mbinu ya kilimo ambayo ina faida kubwa kwa mkulima, huku akiwa amewekeza kwa kiasi kidogo sana katika kukabiliana na wadudu na magonjwa na kuepuka kuwa na mazao yenye ubora wa chini.

Jumamosi, 11 Januari 2014

HAYA NDIO MAGONJWA YANAYOTIBIWA KWA MATUMIZI YA ASALI




 
1. Ugonjwa wa viungo/maumivu na uvimbe.
2. Kukatika kwa nywele.
3. Ukungu wa miguu.
4. Maambukizo kwenye kibofu cha mkojo.
5. Maumivu ya jino.
6. Lehemu (Cholestral).
7. Ugumba
8. Mchafuko wa tumbo.
9. Ugonjwa wa moyo
10. Shinikizo la damu.
11. Kinga ya mwili.
12. Ukosefu wa nguvu za kiume.
13. Flu.
14. Umri wa kuishi.
15. Chunusi.
16. Kuumwa na wadudu (kwa washawasha) wenye sumu.
17. Madhara ya ngozi.
18. Kupungua kwa uzito.
19. Saratani.
20. Uchovu mwilini.
22. Harufu mwilini.
23. Kupungua kwa usikivu.




CHANZO:  FANOPRODUCTS

Ijumaa, 10 Januari 2014

AINA KUMI YA VYAKULA VINAVYOONGEZA UWEZO KATIKA TENDO LA NDOA


Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili.
Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume na kuacha idadi ya wanawake wanaokabiliwa na tatizo hilo kwa mujibu wa uchunguzi kubaki na asilimia 13.
Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili.
Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina kumi ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa. Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:
PILIPILI
Pilipili zilizocheshwa zimetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa usambazaji damu mwilini, ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo unaoweza kumfanya mtu akawa na hisia kali za kimapenzi. Kwa msingi huo, ni vema kwa wale wanaokabiliwa tatizo la uwezo wa kufanya mapenzi wakatumia pilipili si kwa wingi bali kwa kiwango stahili, ili waamshe hisia zao.

PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.

NDIZI
Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa.

CHOKOLETI
Ulaji wa Chokoleti huongeza uchangamfu mwilini na, hivyo kumuwezesha mtu anayeshiriki tendo la ndoa kuwa na mguso sahihi kwenye fikra zake, jambo litakalomuwezesha kupokea hisia za mapenzi kwa urahisi zaidi ya mtu ambaye anakwenda kwenye uwanja wa sita kwa sita akiwa mchovu wa mawazo.

CHAZA NA PWEZA
Aina hizi za samaki zinazovuliwa baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.
POMEGRANATE
Ni aina fulani ya matunda mekundu yanayofananana na apple. Haya yatajwa kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa.

MVINYO MWEKUNDU
Mvivyo mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa, hivyo ni muhimu kunywewa hasa na wale ambao wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kurudia tendo. 

MBEGU ZA MATUNDA
Mchangayiko wa mbegu mbalimbali za matunda, mfano tikiti, maboga husaidia kuondoa ACID mwilini na kumfanya mtu ajione ni mwenye afya njema.

VANILLA
Vanila husaidia kuamasha hamasa mwili.
Mwisho wa aina hizi za vyakula ni TIKITI MAJI ambalo linatajwa kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuusaidia mwili kuwa na nguvu za kutosha kufanya tendo la ndoa.

manyandahealthy@gmail.com

Alhamisi, 9 Januari 2014

SOMO LA LEO KWA WAZAZI: Tatizo la kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu na jinsi ya kulitatua‏



Tatizo la kukosa choo watoto wadogo au kuwa na choo kigumu na jinsi ya kulitatua
Watoto wadogo hasa wale ambao bado wananyonya na ndio 

kwanza wamenzishwa vyakula vinginevyo zaidi ya maziwa, mara nyingi hupatwa na choo kigumu au kukosa choo kabisa (constipation). Hali hiyo huanza pale mtoto anapoachishwa maziwa ya mama na kuanza kunyweshwa maziwa ya kopo au
mengineyo au anapoanzishwa kula vyakula vingine zaidi ya maziwa. 

Mara nyingi watoto wanaonyonya maziwa ya mama huwa hawasumbuliwa na tatizo hilo, bali tatizo hilo huanza kujitokeza pale wanapoanza kulishwa vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama.

Pia mama ambaye tayari mwenyewe anasumbuliwa na tatizo la kukosa choo, huenda mwanae pia akasumbuliwa na tatizo hilo.
Mtoto mwenye tatizo la kukosa choo huwa anapata choo wa shida huku akisumbuliwa na tumbo na kupata choo kigumu. Wakati mwingine hulia wakati akipata choo huku akijiminya na kukunja uso.
 
Muone daktari iwapo mtoto ana umri wa chini ya mwezi mmoja na hajapata choo kwa siku 4.
Iwapo mtoto wako mchanga au mdogo ana tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu kwanza wasiliana na daktari au mpeleke hospitalini ili upate ushari wa daktari. 


Pia unashauriwa kujaribu njia zifuatazo:

1. Jaribu kumpa mtoto wako maji safi na salama kuanzia mililita 60 hadi 120 milimita kwa siku. Punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao inavyokuwa. Ni bora maji ya mtoto yachemshwe na kufunikwavyema.
2. Iwapo maji hayasaidii, jaribu pia kumpa juisi za matunda. Mpe mtoto wako juisi ya tufaha (apple), pea au prune iliyotengenezwa kwa kutumia maji salama na safi kila siku. Anza kwa mililita 60 hadi 120 kwa siku na punguza au ongeza kiasi hicho kwa kuzingatia jinsi hali ya mwanao
inavyokuwa.
3. Jitahidi kumpa mwanao chakula chenye ufumwele (fiber). Iwapo mwanao ameanza kula vyakula vigumu, basi mpe vyakula vyenye ufumwele kuliko vyakula vyenye wanga, kama vile tumia unga wa shayiri au tunda la apple na pea lililopondwapondwa vyema na kuwa kama uji. Epuka kumpa mtoto cereal ya mchele au uji wa mchele kama anatatizo la kukosa choo au kufunga choo.
4. Jiepushe kumpa mtoto wako vyakula vyenye wanga na sukari na vyakula vinavyotengenezwa kwa unga uliokobolewa.
5. Mpake mwanao mafuta kidogo sehemu inayotoka choo kikubwa ili kurahisisha utokaji wa kinyesi. Usitumie mafuta ya madini (mineral oil) au dawa za kulainisha choo na za kuharisha katika kutibu tatizo hilo la kukosa choo la mtoto.
6. Kukosa choo watoto wadogo mara chache huwa kunasababishwa na magonjwa kama vile Hirsch sprung ugonjwa wa kumea neva katika utumbo, au Cystic
Fibrosis. Muone daktari au mpeleke mtoto wako hospitalini kama tatizo hilo la kukosa choo linaendelea hata baada ya kubadilisha aina ya chakula cha mtoto au linaambatana na dalili nyingine kama vile kutapika au mtoto kukosa utulivu na kuhangaika.
7. Kuna baadhi ya watoto wanakosa choo au kuwa na choo kigumu kutokana na kutumia maziwa ya ng’ombe. Iwapo umetumia dawa na umefuata maelekezo ya kuondoa ukosefu wa choo na hukufanikiwa. Katisha kumpa mtoto maziwa ya
ng’ombe kwa siku mbili au tatu, baada ya siku hizo iwapo bado hajaacha choo badi endelea kumpa maziwa hayo, na pengine tatizo hilo halisababishwi na maziwa ya ng’ombe.
8. Muogeshe au muweke mwanao katika beseni la maji ya uvuguvugu na hakikisha maji yanafika hadi kifuani. Mkande mtoto tumbo lake wakati akiwakatika maji na njia hiyo husaidia kulegeza misuli ya mwili wa mtoto, na kumsaidia kupata choo kwa urahisi.
Asante kwa kusoma kwa ushauri na kubadilishana mawazo karibu sana.

Usikose Somo linalokuja

Imeandaliwa na 
Buberwa Robert

JALI AFYA YAKO: HAYA NI MAMBO MUHIMU AMBAYO HUTAKIWI KUYAFANYA MARA BAADA YA KULA CHAKULA.



Kama tulivyoambizana kuwa blog hii itakuja na mambo yanayojulikana lakini hayafanyiwi kazi kwa kuwa watu wamezoea tu kuishi basi leo natoa somo hili ili kukukumbusha usifanye haya wakati umemaliza kula ili usijekupata matatizo.


1. USILALE BAADA YA KULA
Usilale pindi tu mara baada ya kula, kwani chakula ulichokula hakitaweza
kusagwa vizuri na huweza kusababisha vidonda vya tumbo(Ulcers) na
magonjwa mengine ya kuambukiza kwenye utumbo mdogo. 
 2. USINYWE CHAI
iwe mchana au usiku, usinywe chai. Kwa mujibu wa utafiti, majani ya chai
yana kiwango kikubwa cha tindikali (Tannic acid), hivyo unapokunywa chai
tindikali hiyo hufanya protini iliyo kwenye chakula ulichokula kuwa ngumu
na hivyo kutosagika tumboni haraka, matokeo yake ni mtu kukosa choo kwa
siku kadhaa. 

 3. USIOGE
Usioge baada ya kula, oga kabla ya kula. Inaelezwa kuwa unapooga baada ya
kula, mtiririko wa damu huongezeka zaidi sehemu za mikono, miguu na mwili
na kusababisha damu kupungua sehemu za tumboni. Damu inapopungua tumboni
maana yake ni kudhoofika kwa mfumo wa usagaji chakula tumboni. 

4. USILE MATUNDA
Usile matunda baada ya mlo kwani ulaji huo hulifanya tumbo kujaa hewa na
matokeo yake kusababisha gesi tumboni. Kula matunda saa moja au mbili
kabla au baada ya kula chakula chako. Kula matunda muda mfupi tu mara
baada ya kula chakula ni kosa ambalo linafanywa na watu wengi na huonekana
ni sawa. Nakushauri ndugu yangu usiseme aah huyu naye sasa nimekula
halafu kazini natakiwa haraka, nenda kale matunda yako kazini jipe saa
moja au mbili halafu ibia dakika 3 kula matunda yako. Mwisho utaambiwa
kuna virutubisho shilingi lakini tisa utashangaa, wakati uharibifu wa
mwili unaufanya mwenyewe.
 5. USITEMBEE MARA BAADA YA KULA
Kutembea tembea mara baada ya kula husababisha mfumo wa usagaji chakula
kukosa uwezo wa kunyonya virutubisho vilivyomo kwenye chakula tunavyokula.
Badala yake tulia sehemu moja. Inashauriwa usitembee zaidi ya hatua 100.

 6. USIFUNGUE MKANDA GHAFLA
Ni jambo la hatari sana kwa afya ya mtu. Mara baada ya kula, usifungue
ghafla mkanda wa suruali yako, uache kama ulivyokuwa hapo awali kwani kwa
kufanya hivyo kunaweza kusababisha utumbo kujikunja na kuziba.

 7. USIVUTE SIGARA
Sigara ina madhara kiafya, tunashauriwa kuacha kutumia. Lakini inaelezwa
kuwa madhara yake huongezeka mara kumi iwapo mvutaji atavuta mara baada ya
kula chakula. Utafiti wa kimaabara unaonesha kuwa ukivuta sigara moja
baada ya kula ni sawa na mtu aliyevuta sigara 10, hivyo hatari ya kupata
saratani huongezeka kwa asilimia kubwa.


Ndugu yangu binaadamu tuna utashi, akili, maarifa. 
Wanyama wamepewa
akili ndogo zaidi yetu, kwanini wanyama watuzidi, maarifa, akili hadi
utashi sasa. Somo hili linakukumbusha kuwa kwa muda mrefu unaishi bila
kufuata mfumo wa maisha unayotakiwa kuishi.

 Tafadhali kuanzia sasa
unaposoma hapa badili mfumo wako katika ulaji, na nina kushauri kama una
tatizo lolote linalohusiana na tumbo mfano Kukosa Choo, Vidonda vya tumbo,
Gesi Tumboni, Miguu kuwaka moto, Homoni kuvurugika (wakina mama),
kisukari, nguvu za kiume, nguvu za kike, kuumwa sana kichwa, kitambi,
kulala usingizi bila kupenda, hii yote ni sababu ya mifumo mibovu ya
ulaji wa chakula, wasiliana nami kwa ushauri na kupata virutubisho
vitakavyokurekebisha na kurejea katika hali yako kama zamani.

Maoni yako ni muhimu.

Imeandaliwa na Buberwa Blog