TUNAAMBIWA
kuwa kuishi vizuri ni pamoja na kula chakula bora na sahihi. Pia, mtu
anayeishi vizuri ni yule ambaye hasumbuliwi na maradhi hatari na njia
pekee ya kuulinda mwili dhidi ya maradhi hatari ni kujua ipasavyo na
kuvitumia vyakula bora pamoja na kufanya mazoezi.
Katika
makala yafuatayo, nitakuorodhoshea baadhi ya vyakula vinavyotajwa kuwa
bora (super foods) ambavyo faida zake mwilini zimeanishwa. Kwa mlaji,
linakuwa jambo la busara kujua faida ya kila chakula unachoingiza
tumboni.
Kwa
mujibu wa mwandishi wa makala kuhusu vyakula hivi bora, Bw.Hakeem
Rahman, hivi ni vyakula vinavyowafanya “wenye afya nzuri kuendelea kuwa
na afya nzuri zaidi na wenye afya mbovu, kuwa na afya nzuri.”
SAMAKI
Wana
virutubisho aina ya Omega 3 ambavyo huulinda moyo dhidi ya maradhi.
Samaki pia wana virutubisho vinavyomuongezea mlaji uwezo wa kukumbuka
(memory), kuna virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na kansa mwilini,
kuongeza kinga mwilini na kuondoa mafuta mabaya mwilini (Bad
cholesterol). (unashauriwa kula samaki kwa wingi kadiri uwezavyo).
Baadhi
ya virutubisho muhimu vinavyopatikana kwenye samaki ni pamoja na
vitamini D, vitamin 12, Vitamini B3, vitamini B6, Omega 3 Fatty Acids,
Protini na madini mengine mengi.
KAMBA (PRAWNS)
Samaki
aina ya kamba hutoa kinga dhidi ya maradhi ya moyo, shinikizo la damu
(High Blood Pressure), huboresha ‘mudi’ ya mtu, huondoa mfadhaiko wa
akili na hupunguza maumivu ya viungo. (unashauriwa kula kamba japo mara
moja kwa wiki.
KARANGA
Unaweza
ukazidharau karanga, lakini zina faida kubwa mwilini. Miongoni mwa
faida zake ni pamoja na kuimarisha afya ya moyo, hupunguza kolestro
mbaya mwilini na kuongeza kolestro nzuri. Mafuta mazuri yaliyomo kwenye
karanga hupunguza shinikizo la juu la damu na huponya magonjwa ya moyo
na hupunguza uzito. Faida zote hizi unaweza kuzipata kutoka kwenye
karanga au siagi iliyotengenezwa kutokana na karanga (peanut butter).
(unashauriwa kula kiasi kadhaa kila siku, hasa za kuchemsha ndiyo
nzuri).
KAROTI
Miongoni
mwa faida nyingi za karoti ni pamoja na kushusha kolestro mbaya
mwilini, kupunguza unene, kuimarisha nuru ya macho, kuimarisha shinikizo
la damu, inatoa kinga kwenye figo na inaimarisha sukari mwilini. (kula
kadiri unavyoweza, mbichi au zilizochemshwa).
MAHARAGE YA SOYA
Haya
ni maharage bora kabisa ambayo yana faida nyingi mwilini, ikiwemo
kushusha shinikizo la damu, kuimarisha sukari mwilini, kupambana na
ugonjwa wa kisukari, figo, moyo, kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa kansa
ya kibofu na magonjwa mengine ya wanawake.
PAPAI, TIKITI MAJI
Miongoni
mwa matunda muhimu mwilini ambayo hata mgonjwa wa kisukari anashauriwa
kuyala ni pamoja na papai na tikitimaji ambayo yanaelezwa kuwa na
kiwango kikubwa cha kamba lishe (fibre) na hivyo kutoa mchango mkubwa
sana katika kuimarisha kiwango cha sukari mwilini. (kula kiasi cha moja
katika ya matunda hayo mawili, kila siku).
Itaendelea wiki ijayo.Chanzo GPL
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni