mapishimapishi

mapishimapishi

Jumanne, 7 Januari 2014

SOMO LA LEO: UMUHIMU WA ASALI, FAHAMU ASALI HALISI NA FEKI, SOMA HAPA.


TUNAFAHAMU kwamba asali ina umuhimu mkubwa sana katika mwili wa binaadamu, lakini watu wengi wamekuwa wakipigwa kwa kuuziwa asali feki, sasa leo nimeona niwape darasa wanunuzi wa asali ili wasiweze kununua asali feki. 

Maana sehemu nyingi hasa Kariakoo, wafanyabiashara wamekuwa wakiuza asali ambayo haina ubora kwa kuchanganya maji na sukari guru. 
Njia ya kwanza, chukua njiti ya kibiriti kisha ichovye sehemu yenye baruti kwenye asali unayotaka kuinunua, kisha iwashe njiti hiyo kwa kutumia kibiriti chako, ikiwaka, ujue hiyo ni asali kweli. 
Njia ya pili, dondosha asali chini katika mchanga, ukiona sehemu ya mchanga iliyolowana ikijikusanya pamoja ujue hiyo nii asali orginal. 
Njia ya tatu, Chukua karatasi jeupe, dondoshea asali njia juu yake, kama ikichelewa kutokea upande wa pili, ujue hiyo asali safi na inafaaa kwa matumizi ya binaadamu.
Bado kuna njia nyingine ambayo hutumiwa na baadhi ya watu, kama vile kuimwaga katika kiganja cha mkono wako, ukiona tone la mwisho linabakia kwenye chupa kuja mkononi, hiyo ni asali nzuri. 
Pia wengine huangalia kama ikiwa kwenye chupa huwa inatengeneza alama yenye mfano wa korosho. 
Nadhani hutaibiwa tena kwa kuuzia asali feki.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni