mapishimapishi

mapishimapishi

Jumatatu, 6 Januari 2014

NAMNA YA KUANDAA MISHKAKI YA MAANDAZI

Napenda sana kupika maandazi,kila ninapokanda unga wa maandazi nahisi kama ninashika udongo mfinyazi na akili yangu uwaza kubumba,kukata na kutengeneza vitu au maumbo mbalimbali.
031
Mishkaki ya maandazi  ni kama maandazi mengine yoyote chatofauti nikwamba maandazi haya huwekwa kwenye mti au mdenge wa mshkaki nahivyo hufanana sana na mshkaki
Unaweza andaa maandazi haya kwakutumia recipe yoyote ya maandazi unayopenda.Chagua recipe yoyote yamaandazi hapa jikoni.
Njia
1.Kanda unga wa maandazi  adi uwe tayari kwa kusukuma
2.Gawanya unga wako mara nne zaidi kutokana na wingi wake,kisha sukuma ili kupata chapati nene
  • Chapati ikiwa nyembamba ,ukikaanga maandazi yatajaa hewa ndani na yatachomoka kwenye mti /mdenge wa mshkaki
3.kwakutumia kisu kikali kata unga wako katika vipande virefu vyembamba (kwa urefu).kisha chukua kipande kimoja na ukikate vipande vidogo vidogo (kwa upana) .Utapata maandazi madogo madogo katika umbo la pembe nne.
018
4.Pakaa unga wa ngano kwenye mti wa mshakaki ,kisha Chomeka maandazi hayo kwenye mti huo  uku ukuicha nafasi yakutosha kila baada ya andazi moja ili kutoa nafasi ya andazi kuumuka wakati wakukaanga .
5.Kaanga kama unavyokaanga maandazi kawaida.Weka kwenye chujio yadondoshe mafuta kisha weka juu ya chombo kilichotandikwa karatasi ili kuondoa mafuta yaliobaki juu.Maandazi tayari kwa kula.
Muonekano wa maandazi haya huvutia sana. Ni vyema kua na utofauti katika upishi wako,mpe mlaji kitu chakushangaa na kufuraia anapokula.
Naamini ukiandaa maandazi haya siku yakwanza familia yako itakua na mengi yakusema.kama mtoto hawapendi kula basi hii ni namna nyingine yakumvutia mtoto kula.

MUONEKANO MZURI WA CHAKULA HUMVUTIA MLAJi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni