Mgahawa wa kwanza maalum kwaajili ya mbwa na paka uitwao ‘Pets Deli’ umefunguliwa huko Berlin, Ujerumani.

Kati ya vyakula 
vinavyopatikana katika menu ya mgahawa huo ni pamoja na beef, bata 
mzinga, cupcakes, wali, viazi bila kusahahu nyama ya Kangaroo.

Mgahawa huo 
uliofunguliwa katika kipindi cha Christmas mwaka jana 2013, vyakula vya 
wanyama hao vinauzwa kuanzia €3 hadi €6 (6500-13000Tsh).

Katika mgahawa huo 
kuna sehemu imetengwa kwaajili ya wamiliki wa wanyama hao kupata kahawa 
wakisubiri mbwa na paka wao wapatiwe huduma.


Mmiliki wa mgahawa 
huo David Spanier (31) alisema alipata wazo baada ya kugundua rafiki 
yake hua anashindwa kutumia vyakula vya supermarket kwaajili ya wanyama 
kutokana na kuwa junk food.

Spiner aliongeza kuwa nyama inayoandaliwa ina ubora ambao inaweza hata kuliwa na binadamu bila tatizo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni