Sehemu ya Kwanza..
Kama
ada kama dawa blog yetu inajieleza kwamba itakuwa inakumbusha au kutoa elimu ya
vitu tunavyovijua lakini tumesahau au hatufuatilii, nah ii yote ni kutaka
kukupa changamoto wewe msomaji ili uweze kufikiri njia nyingine ya kuweza
kujiongezea kipato kupitia kilimo pia.
Upandikizaji hujumuisha aina mbili za mimea.
Unachukua mmea mmoja ambao unadhani hauna tija nzuri, na sehemu ya mmea
mwingine ambao una ubora zaidi na kupandikiza kwa kukata na kufunga pamoja ili
kupata mbegu bora zaidi.
Kwenye shamba la bwana Buberwa Robert, atakuwa na
kitalu chenye zaidi ya miche 1500 ya miparachichi, ikiwa inasubiri kufikia
wakati wa kupandikiza.
Mbinu anayotumia
Kukusanya kokwa za parachichi kutoka maeneo ya
sokoni; atakachofanya ni kuhakikisha tu kuwa mbegu hiyo ni safi, haijaathiriwa
na magonjwa na itaota. Baada ya hapo huchagua zile zenye muundo mzuri na
kuzipanda kwenye boksi au kwenye sehemu ya kitalu. Baada ya kuota ataziotesha kwenye
makopo, au kwenye viriba kisha kuendelea kumwagilia maji mpaka zinapokuwa na
umbo usawa wa penseli. Upandikizaji ni lazima ufanyike wakati mmea umefikisha
unene wa penseli. Kupandikiza kwa kutumia chipukizi lililolingana na mche
unaopandikizia ni njia yenye mafanikio zaidi.
Upandikizaji ni lazima ufanyike wakati ambao
mizizi bado ni laini. Pandikizi litakalotumika wakati wa kupandikiza ni lazima
lisiwe katika hatua ya ukuaji kwa wakati huo, na ni lazima umbo liwiane na mti
linapopandikizwa kuzuia maji yasipotee na kusababisha pandikizi kukauka.
Mapandikizi ni lazima yatokane na aina ya
parachichi ambazo zimeboreshwa kama vile HASS,
FUERTE au PUEBLA . Kwa wale wakulima ambao mmea utatoa majani mapya. wana
mkataba na Africado, watahitaji kupata mapandikizi kutoka kwenye miti ya HASS. Hii ina maanisha kuwa mkulima
anayetaka kuanzisha kitalu kwa ajili ya kupandikiza ni lazima apande walau miti
5 ya parachichi aina ya HASS ili
kupata mapandikizi.
Njia ya kupandikiza ina ufanisi zaidi na ni
rahisi kuliko kupanda miche upya, kwa kupandikiza inagharimu chini ya asilimia
75, kuliko kupanda miche upya na kuweza kupata aina ambayo inastahimili magonjwa.
Wakulima pia wamekuwa na rekodi nzuri ya ongezeko la mavuno kutokana na mimea
waliyopandikiza, pamoja na upungufu wa matumizi ya madawa.
Wakulima ambao wanafanya kazi zao chini ya
CARITAS Njombe sasa wanaona faida kubwa inayotokana na kupandikiza, wameamua
kuwekeza kwenye utaalamu huu na kuwa na miche mingi kwenye vitalu vyao. Hii ni
mbinu ya kilimo ambayo ina faida kubwa kwa mkulima, huku akiwa amewekeza kwa
kiasi kidogo sana katika kukabiliana na wadudu na magonjwa na kuepuka kuwa na
mazao yenye ubora wa chini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni